Na COSTANTINE MATHIAS, Matukio Daima Geita.
MKULIMA wa Pamba kutoka Kijiji Cha Bukondo, Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita, Kusekwa Matonange ameibuka kuwa mkulima hodari mara baada ya kuvuna kilo 3024 za Pamba katika ekari moja kwenye msimu wa Kilimo 2024/25.
Akizunguma na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea nyumbani kwake, mkulima huyo hodari amesema kuwa wakati anaandaa shamba la kulima aliandaa ekari moja ambayo imevuna Pamba yenye uzito wa Tani 3 sawa na kilo 3024 hali ambayo imempa Mafanikio makubwa baada ya uvunaji.
Kutokana na kuwa mkulima hodari, Matonange amejishindia kiasi cha Shilingi Mil. 7, fedha ambayo imetolewa na Bodi ya Pamba (TCA) kama motisha Kwa kutambua juhudi za wakulima wa Pamba wanaozingatia kanuni za kilimo cha pamba na kuzalisha kwa tija
Pamoja na pesa taslimu kwa Mshindi, Bodi ya Pamba imewazawadia wakulima wawili kila wilaya majiko ya Gesi ili kuunga Mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kutumia nishati safi na kutunza Mazingira.
Mwisho.
0 Comments