Thabit Madai, Matukio daima Media.
Zanzibar.Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia wajasiriamali kwenye sekta ya utalii kuwa endapo atapata ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa Zanzibar atahakikisha wananufaika na sekta hiyo na kuondoshewa changamoto wanazozikabiliana nazo
Dkt Mwinyi ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na makundi mbalimbali ya utalii katika ukanda wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake visiwani Zanzibar
Amewahakikishia makundi hayo wakiwemo Beach Boys kuwa serikali yakr itahakikisha inawawekea mazingira rafiki na utambuzi rasmi ili kupata fursa mbalimbali na kuendesha shughuli zao za kujikwamua kiuchumi
0 Comments