Botswana imetangaza sikukuu ya kusherehekea ushindi wa nchi hiyo katika mbio za mita 4x400 wanaume kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia mjini Tokyo, baada ya taifa hilo kuwa la kwanza la Afrika kushinda mashindano hayo.
Rais Duma Boko alipongeza medali ya dhahabu kama "ushindi wa kihistoria wa Afrika", katika hotuba ya mtandaoni ya kusifu timu kwa namana walivyoshiriki.
Alitangaza Jumatatu, Septemba 29, kama sikukuu ya kusherehekea mafanikio hayo - siku moja kabla ya siku ya uhuru wa nchi.
Siku ya Jumapili, timu ya Botswana ya Lee Bhekempilo Eppie, Letsile Tebogo, Bayapo Ndori na Busang Collen Kebinatshipi waliishinda Marekani, ambao ni washindi wa mataji 10 ya mwisho ya dunia, katika mbio zilizokimbiwa huku mvua ikinyesha. Afrika Kusini ilishika nafasi ya tatu.
"Nitakuwa na uhakika wa kumwambia kila mtu, almasi ya asili ya Botswana sio tu ardhini, ni wanariadha wetu Bingwa wa Dunia," rais alisema, akizungumza kutoka New York ambako anahudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
0 Comments