Header Ads Widget

WAKULIMA NA WAFUGAJI WATAKIWA KUZINGATIA UBORA WA VIWATILIFU NA DAWA ZA MIFUGO

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA MBEYA

Katika kuhakikisha tija katika kilimo na ufugaji inafikiwa nchini, wakulima na wafugaji wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya viwatilifu na dawa, huku wakiepuka bidhaa zisizo na ubora ili kulinda afya ya mimea, mifugo na binadamu.


Wito huo umetolewa na Afisa Ugani kutoka kampuni ya JUBAILI AGROTEC, Bwana Elineo Chaula, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya kilimo yaliyohitimishwa leo katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya.



Bwana Chaula amesema baadhi ya wakulima wamekuwa wakitumia viwatilifu visivyo na ubora ama kuvifuata bila ushauri wa kitaalamu, jambo linalohatarisha uzalishaji na afya ya walaji.


"Ni muhimu kila mkulima atumie viwatilifu kwa ufasaha, kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo na kuhakikisha bidhaa wanazonunua zina ubora na usajili unaotambulika kisheria," amesisitiza Chaula.

Kwa upande wake, Afisa Mifugo kutoka kampuni hiyo, Dkt. Boazi Peter Mwaseba, amesema ufugaji wa kisasa unahitaji nidhamu na uelewa wa matumizi ya dawa ili kuepuka madhara kwa mifugo na walaji wa mazao yake.


"Tunawasihi wafugaji wasiwe na mazoea ya kununua dawa ovyo mitaani au kutumia bila vipimo sahihi. Wawatumie wataalamu wa mifugo ili kupata tiba na chanjo zinazofaa," amesema Dkt. Mwaseba.


Maafisa hao wametoa rai kwa wadau wote wa sekta ya kilimo na mifugo kuwa sehemu ya mapinduzi ya kilimo endelevu kwa kuzingatia matumizi bora ya pembejeo, ikiwemo viwatilifu na dawa za mifugo, ili kuongeza uzalishaji na kulinda afya za watumiaji wa bidhaa za kilimo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI