TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewapitisha wagombea wa Vyama 17 kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isipokuwa mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina.
Majina ya wagombea hao yamebandikwa leo Agosti 27,2025 katika ubao wa matangazo uliopo katika ofisi za INEC
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa INEC, Kailima Ramadhan, vyama hivyo pekee ndivyo vilivyokidhi vigezo vilivyowekwa na tume hiyo ambapo kampeni za uchaguzi zitaanza rasmi kuanzia Agasti 28.
0 Comments