Mamlaka ya udhibiti wa safari za nga ya India imebaini kuwa kulikuwa na ukiukaji wa kanuni za usalama 51 katika Air India wakati wa ukaguzi wake wa kila mwaka wa anga mwaka jana.
Matokeo hayo yamekuja kufuatia ajali ya ndege ya Air India Boeing 787 iliyoua watu 260 mwezi uliopita, ingawa hayakuhusishwa na tukio hilo.
Wakaguzi hao walisema kuwa masuala saba ya usalama yaliyoripotiwa yalikuwa mazito sana, lakini hawakutoa maelezo.
Air India ilisema ilikuwa "wazi kabisa" wakati wa ukaguzi wa murugenzi mkuu wa usafiri wa anga (DGCA) mnamo Julai, ambao ulifanyika kama sehemu ya ukaguzi wa kawaida ili kuboresha shughuli za ndege.
Msemaji alisema ni kawaida kwa mashirika yote ya ndege kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara ili kutathmini na kuboresha shughuli zao.
0 Comments