NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMA MWANZA.
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Mashariki imetoa onyo kwa wafugaji, wakulima na wavuvi wanaotumia dawa bila kuzingatia kanuni, hatua hiyo inaweza kuleta athari kama dawa hizo zinaweza kutumika vibaya.
Hayo yamebainishwa Agosti 8, 2025 katika maonesho ya wakulima nane nane Jijini Mwanza na Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki, Aggrey Muhabuki, na kueleza kuwa Matumizi yasiyo sahihi ya dawa yanaweza kusababisha kuibuka kwa vimelea sugu, kuharibu ubora wa nyama, maziwa na mayai, Kwa kutumia mazao hayo kabla ya muda ambao mazao hayo yanastahili kutumika.
Muhabuki ameeleza kuwa TMDA imetumia maonesho hayo kutoa elimu ya ana kwa ana kwa wadau, ikiwemo namna sahihi ya kutumia dawa, vifaa tiba na viuwa simu pamoja na kukuusanya taarifa kutoka kwa wafugaji ili kupanga ratiba ya mafunzo yatakayotolewa kwenye maeneo yao.
“Sisi tumeshiriki katika maonesho haya maonesho ya Saba ya Kanda ya Ziwa magharibi, yaliyojumiisha Mikoa ya Kagera, Mwanza pamoja na Geita, na sisi ofisi yetu imeweza kufika hapa na watalaamu waliobobea ili kutoa elimu Kwa wananchi
Mhabuki aliongeza kuwa dawa zinazotumika kunenepesha au kutibu mifugo zinapaswa kuzingatia muda maalumu wa kusubiri kabla ya mazao husika kutumika kwa chakula, ili kuepusha madhara ya kiafya.
“Tutapanga mpango wa kuwatembelea mara kwa mara, kwa sababu elimu ya matumizi sahihi ya dawa ni muhimu katika kulinda si tu afya ya mifugo, bali pia usalama wa chakula na afya ya jamii nzima,”Alisema Muhabuki.
0 Comments