Header Ads Widget

NRA YAJA NA KIPAUMBELE CHA AMANI KUANZA ZIARA MIKOA 10 KUSAKA WADHAMINI.

Na Hamida Ramadhan, MatukioDaima Media Dodoma

MGOMBEA Urais kupitia Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Hassan Almasi, leo amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) huku akitaja kipaumbele chake kikiwa ni amani. 

Mgombea huyo ambaye alifika ofisi za Tume ya Uchaguzi saa 7:55 mchana ambapo aliambatana  na mgombea mwenza Ally Hassan akiwa katika gari lenye namba za usajili T 964 ECB Benz pamoja na T 497 DNR  aina ya Murano. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Almasi amesema hatua inayofuata ni kuanza ziara katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na Visiwani kwa ajili ya kutafuta wadhamini kabla ya kurejea kuwasilisha fomu rasmi kwa wanachama wa chama chake.

“Imani yetu chakwanza ni Mungu, pili ni wapigakura, na tatu ni tume huru ya uchaguzi haya ndio matumaini yetu , " 

Na kuongeaza "Sisi kama chama cha NRA tuko tayari kukosa uongozi kuliko kuingiza nchi katika  machafuko na hayo  ndiyo matumaini makubwa waliyonayo kwa chama chetu,” alisema Almasi.

Mgombea huyo alikuwa ameambatana na mgombea mwenza wake, Ally Hassan, ambapo walikamilisha mchakato wa uchukuaji wa fomu hiyo saa 7:21 mchana.

Hata hivyo Chama cha NRA kinatarajiwa kuwa miongoni mwa vyama vitakavyowasilisha wagombea wake katika uchaguzi mkuu ujao, huku kikiahidi kampeni zenye amani na mwelekeo wa kuleta mabadiliko ya kweli kwa Watanzania.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI