Mwisho uliowekwa na Tume huru ya Uchaguzi INEC kwenye zoezi la urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi za udiwani umeacha gumzo Kata ya Mindu, Morogoro, baada ya Zuberi Mkalaboko – mtangazaji wa EFM na kada wa CCM – kurejesha fomu zake kwa kishindo.
Kijana huyo anayegombea kwa mara nyingine, sasa akitetea nafasi hiyo, aliwasili akisindikizwa na umati wa wafuasi waliomshangilia, kuimba na kucheza akijinasibu kama "kiungo wa maendeleo" atakayesaidia kufunga mabao ya ustawi wa wananchi wake kwa kukamilisha pale alipoachia, changamoto kubwa akizipa kipaumbele za ukarabati Miundo mbinu ya barabara, maji, zahanati shule, madaraja na vivuko, fursa za kiuchumi ili kuwaondoa wananchi na utegemezi pamoja na changamoto zilizokwisha Anza kutatuliwa na Serikali ya awamu ya tano.
Mkalaboko alitoa wito kwa wakazi wa Mindu kumpa nafasi ya udiwani, huku akiwataka waendelee kuwa imara nyuma ya Abood kwa ubunge na Samia Suluhu Hassan kwa urais ili iwe rahisi kutatua changamoto za wananchi kwa ushirikiano wa pamoja.
0 Comments