Header Ads Widget

KAPUFI ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UDIWANI KATA YA KITWIRU.

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

IRINGA.Mgombea udiwani wa Kata ya Kitwiru kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Rahim Kapufi leo August 18 amefika katika ofisi ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika kata hiyo baada ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu 2025.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo mgombea udiwani wa kata ya Kitwiru Kapufi ameishukuru kamati kuu ya chama cha mapinduzi CCM kwa kuliteua jina lake na kuwa mgombea udiwani wa kata hiyo huku akiahidi kufanya kampeni za kistaarabu. 

Kapufi alisema kuwa CCM imejengwa katika misingi ya kidemokrasia na kuhemu matakwa ya wanachama na wanachi kwa ujumla kwani matamanio ya wakazi wa eneo hilo lilikuwa nikuona wanapata mgombea udiwani kijana hivyo aliomba wampe ushirikiano kwa kumpa kura nyingi ili akawe mwakilishi wao.

Alisema kuwa anatambua katika kata ya kitwiru ina miradi mingi ya maendeleo iliyokuwa ikisimamamiwa na mtangulizi wake ambapo ameahidi kwa kushirikiana na wananchi atahakikisha inakamilika katika kipindi atakachokuwa muwakilishi wao kama watampa ridhaa.

Aidha aliongeza kusema kuwa anatambua kuwa yeye ni kijana na hivyo anahitaji busara na hekima kutoka kwa wazee katika kuwatumikia wananchi wa Kitwiru.

Ndugu zangu wanaccm na wananchi kwa ujumla tunafahamu tumepita katika mchakato hadi kufikia leo chama kimepitisha jina langu kuwa mgombea udiwani wa kata yetu niwaombe mnipe ushirikiano kumbukeni sisi wote tulikuwa washindi lakini chama kimeteua mmoja ndio awe mgombea niwaombe watia nia wenzangu tuunganishe nguvu zetu kuhakikisha CCM inapata ushindi, alisema Kapusi.

Aidha amewaomba wanaccm wa kata ya Kitwiru kuendelea na ushirikiano katika kuzitafuta kura nyingi za Rais, Mbunge na Diwani ili kukiletea ushindi chama cha mapinduzi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Kitwiru Juma Kinyonga amewataka wanaccm wa kata hiyo kuvunja makundi na kuunganisha nguvu katika kuzitafuta kura za chama hicho.

Alisema katika mchakato wa kura za maoni kulikuwa na makundi mbalimbali ambayo kila mmoja alikuwa na mgombea wake kutokana na chama kurudisha jina la mteule mmoja hivyo makundi yanapaswa kuvunjwa na kuwa kitu kimoja.

Kinyonga alisema wanaccm wa kata ya kitwiru wamekuwa na umoja yanapokuja maendeleo ya chama chao nakuendelea kuendelea kuwahamasisha kuendeleza umoja huo hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika.

Aidha aliwataka wanaccm kumuelekeza mambo mbalimbali ya ndani na nje ya chama hicho badala ya kumpelekea maneno ya uchonganishi yatakayoleta mpasuko wa chama hicho.

Wanaccm niwaombe tumpe ushirikiano huyu kijana, ni mtoto mdogo anahitaji maarifa yetu, upendo na ushirikiano tukianza kumpekea majungu tutampoteza na kukiletea chama chetu mpasuko jambo ambalo katika kata ya Kitwiru hatutalikubali, alisema mwenyekiti huyo.

Aidha aliongeza kwa kumtaka mgombea udiwani wa kata hiyo Rahim Kapufi kutokuwabagua wanaccm ambao hawakuwa upande wake kwani baada ya mchakato huo kumalizika wanarudi na kuwa kitu kimoja.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI