Header Ads Widget

TANESCO MWANZA KUFUNGA MITA JANJA KWA WATEJA ILI KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA.

 



NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA.


MWANZA, Katika juhudi za kuboresha huduma ya umeme na kuhakikisha usambazaji  unaendelea kuwa bora, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Mwanza limeanza zoezi la kufunga mita janja (smart meters) kwa wateja wake.


Akizungumza na Matukio Daima Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mwanza, Alistidia Clemence, amesema kuwa  lengo la ufungaji wa mita hizo ni kudhibiti upotevu wa limoti na kuharibika kwa mita za zamani, ambazo zimekuwa zikileta usumbufu kwa wateja. 


"Tumeamua kubadilisha mita za kawaida na kuzibadilisha kuwa mita janja (smart meters), ambazo zitakuwa suluhisho kwa wateja wetu na kutatua changamoto na kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa ufanisi.," alisema Clemence.


Clemence ameeleza kuwa hadi sasa wamefanikisha kufunga mita 1889 kwa wateja wa single-phase na three-phase ambapo Mita hizo zinafungwa kwa Kufata utaratibu wa mtaa, na sio kwa mteja mmoja mmoja, ili kuhakikisha usawa na ufanisi katika usambazaji wa huduma. 


Aidha Clemence alisisitiza kuwa hatua hii itaondoa changamoto ya kujaza umeme, hususani katika kipindi cha mvua, kwani wateja sasa watakuwa na uhakika wa kumiliki umeme kwa wakati.


"Zoezi la kubadilisha mita janja ni bure na hakutakuwa na gharama yoyote inayohusiana na zoezi hilo Wananchi wanahimizwa kufuata utaratibu na kuhakikisha wanapata umeme kwa njia halali." Alisema Clemence".


Kwa upande mwingine Clemence amefafanua kuwa Tanesco imeendelea Kupambana na watu ambao wanaojiunganishia umeme kwa njia zisizo halali kupitia vishoka hivyo kuwataka watu hao  kuachana na tabia hiyo kwani kuna njia rahisi ya kupata umeme.


"Kwa wananchi ambao wanapitia kwa vishoka kupata huduma za umeme, tunawaomba wasikubali kurubuniwa, Kama kuna mtu yeyote ambaye alijiunganishia umeme kwa njia isiyo halali, anahimizwa kuja kujisalimisha ili aweze kupata huduma kwa njia sahihi," alisema Clemence.


Aidha alisisitiza kuwa, Tanesco itachukua hatua kali dhidi ya wateja wanaobainika kujiunganishia umeme kwa njia haramu, na faini zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.


Mwisho 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI