Header Ads Widget

EWURA CCC YAPONGEZWA ,YATAKIWA KUIMARISHA HUDUMA VIJIJINI


 Hamid Ramadhan, MatukioDaima Media Dodoma

BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC)limeshauriwa  kuimarisha elimu kwa wananchi hususani wanaoishi Vijijini  ili kuongeza uelewa wa huduma hizo muhimu kupitia maonyesho ya Wakulima  nanenane.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule,ameyasema hayo jijini Dodoma  alipotembelea banda la Baraza hilo katika Maonesho ya  Kitaifa ya Wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini.


Aidha Senyamule ,amesisitiza umuhimu wa Baraza hilo ni kuongeza kasi ya kutoa elimu ya matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira, ufuatiliaji wa bei za mafuta na huduma za maji na umeme, ili wananchi wa vijijini waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo na biashara kwa tija zaidi

"Katika kuongeza ufanisi wa huduma hizo, nawaagiza wataalamu wa EWURA kutumia majukwaa  hasa Jukwaa la Nanenane 

Maonesho ya Nanenane, yanayofanyika kila mwaka, yamekuwa kiunganishi muhimu kati ya serikali, wakulima na wadau wa maendeleo,"Amesema

Awali,Mkuu huyo wa Mkoa amepokea maelezo kutoka kwa Afisa Uelimishaji na Uhamasishaji wa EWURA CCC, Lugiko Lugiko, kuhusu huduma zinazotolewa na Baraza hilo, ikiwemo kusikiliza na kushughulikia malalamiko ya watumiaji wa huduma za mafuta, gesi, umeme na maji hatua inayotajwa kuwa ni chachu ya kuongeza ufanisi na uwazi katika sekta hizo.

Lugiko ameeleza kuwa ushiriki wa EWURA CCC katika Maonesho ya Wakulima mwaka huu ni sehemu ya mkakati wa kusogeza  huduma kwa wananchi, hususani wale wa maeneo ya pembezoni, ambao mara nyingi hukosa taarifa sahihi na mwongozo wa namna bora ya kushughulikia changamoto na malalamiko yanayohusiana na huduma za nishati na maji.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI