Na Shemsa Mussa -Matukio Daima.
WAJUMBE wa mkutano mkuu wa uchaguzi kutoka Umoja wa Wanawake chama cha Mapinduzi UWT mkoa wa Kagera wametakiwa kufahamu, ushindi wa matokeo ya kura za maoni sio ubunge wa nafasi ya viti Maalumu bali ni waliongoza kwa kura za maoni.
Kauli hiyo imetolewa Jana na Msimamizi wa uchaguzi huo, Yasimin Bachu wakati akitangaza matokeo ya kura za kuwapata wagombea wa nafasi hiyo.
Alisema,ushindi huo,ni hatua iliofanywa kwa kura za maoni kumpata kupitia kanuni na mwongozo wa chama,ili kufukia hatua ya ushindi wa nafasi ya viti Maalumu ndani ya mkoa lazima kuweka na jitihada za kuhakikisha ushindi wa majimbo ndani ya mkoa yapatikana ndani ya chama.
Alisema,alisema kura za maoni zilikuwa 1482 kati ya 1483 iliyoharibika ni mojana majina ya wagombea walikuwa nane.
Aidha alisema, wagombea waliochaguliwa wazidiana kwa kura 52 ikiwa Devotha Daniel ameshinda kwa 1308 na Samila Halfan kwa 1256.
Mahindi wa kura za maoni Devotha Daniel aliyeshinda kwa kura 1308kati ya 1482 alisema baada ya ushindi ni jukumu la kwenda kutafuta kura ambazo zitasaidia kufukia nafasi inayowaniwa
"Sio kwamba walioshindwa walikuwa hawafai apana ni kura zimepisha na wao wanafaa na sasa tuweke umoja katika kulinda chama na kujenga nyumba Moja"alisema Daniel
Hata hivyo alisisitiza kwamba nafasi za kugombea kupitia chama cha Mapinduzi CCM zifanyiwe kazi na vijana ili wawze kujenga Taifa na kufanikisha maendeleo.
0 Comments