Header Ads Widget

CHAN 2024: AFRIKA MASHARIKI KUANDIKA HISTORIA?

 

CHAN (African Nations Championship) ni mashindano ya kila baada ya miaka minne yaliyoanzishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa ajili ya timu za Taifa za Afrika. Lengo la mashindano haya ni kutoa fursa kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani za nchi zao kushiriki katika michuano ya kimataifa.

Michuano ya CHAN 2024 itaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania. Hapo awali mashindano hayo yalikusudiwa kufanyika Februari 1-28, lakini yaliahirishwa kwa lengo la kutoa muda zaidi kwa nchi waandaaji kufanya maandalizi.

Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Mwananchi, maandalizi hayahusu viwanja pekee, kama ambavyo watu wanadhani, kuna viwanja vya mazoezi, usafiri wa mashabiki, hoteli, hospitali na mambo mengine mengi yanayohitajika kwa mashindano ya aina hii.

Mashindano ya CHAN 2024 hatimaye yatafanyika Agosti 2 hadi 30 2025. Ni kwa mara ya kwanza CHAN kuaandaliwa na nchi tatu za Afrika mashariki, hiyo hi historia mpya itakuwa imeandikwa, lakini historia hiyo itakuwa bora zaidi ikiwa moja ya timu wenyeweji itahakikisha kombe linabaki katika jumuiya hii.

CHAN 2024

Uganda ama Uganda Cranes

Nchi 19 zinajiandaa kuchuana katika mechi zitakazochezwa Nairobi, Dar es Salaam, Kampala na Zanzibar. Jumla ya michezo 44 imepangwa kuanza na mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Tanzania dhidi ya Burkina Faso jijini Dar es Salaam.

Fainali ya mashindano hayo itafanyika katika uwanja wa Kasarani Kenya wenye uwezo wa kuchukua watu 60,000 ifikapo Agosti 30, huku mchezo wa mshindi wa tatu ukipangwa kufanyika Kampala.

Viwanja vitakavyotumika

Uwanja wa Kasarani, Nairobi – mashabiki 60,000

Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam – mashabiki 60,000

Uwanja wa Taifa Mandela, Kampala – mashabiki 45,000

Uwanja wa Taifa wa Nyayo, Nairobi – mashabiki 30,000

Uwanja wa Amaan, Zanzibar – mashabiki 15,000

Katika droo iliyofanyika Januari 15, 2025 jijini Nairobi, Kenya ilipangwa Kundi A lenye timu ya Morocco na DR Congo, Angola na Zambia.

Tanzania ipo Kundi B pamoja na Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Uganda katika Kundi C ikichuana na Niger, Guinea, Afrika Kusini na Algeria.

Wawakilishi wengine kutoka Kanda ya CECAFA ni Sudan ambao watacheza katika Kundi D pamoja na mabingwa watetezi Senegal, Nigeria na Equatorial Guinea.

Makundi ya CHAN 2024

Kundi A: Kenya, Morocco, Angola, DR Congo, Zambia

Kundi B: Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kundi C: Uganda, Niger, Guinea, Algeria, Afrika Kusini

Kundi D: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Nigeria.

Hisotoria ya CHAN kwa wenyeji

Mashabiki wa Kenya

Wakiwa wanashiriki michuano hiyo kwa mara ya saba, Uganda Cranes hawajafanikiwa kuendelea zaidi ya hatua ya makundi. Uganda imeshirika mwaka 2011, 2014, 2016, 2018, 2020 na 2022.

Kwa mujibu wa CAF, Uganda ndio taifa lililofanikiwa zaidi kutoka kanda ya CECAFA likiwa na mataji 40 ya CECAFA. Hivyo watakuwa na matumaini ya kuongeza kombe la CHAN kwenye kabati lao la makombe mwaka huu wakiwa nyumbani.

Fainali za mwaka huu zitakuwa ni za tatu kwa Tanzania kushiriki baada ya kufanya hivyo mwaka 2009 iliposhirika katika kundi 'A' na kuishia makundi, ikimaliza nafasi ya tatu na pointi nne. Tanzania ikashiriki tena mwaka 2020 na kuishia tena makundi, ilipomaliza nafasi ya tatu kundi 'D' na pointi nne.

Kenya imepata nafasi ya kushiriki michuano ya CHAN 2024 kwa mara ya kwanza, kama mojawapo ya mataifa matatu yatakayoandaa. Fursa hii ya kihistoria inawapa Harambee Stars nafasi yao ya kwanza kuonyesha vipaji vyao.

Historia ya CHAN

Senegal ilishinda CHAN 2022, iliyoshirikisha timu 17

Katika mashindano haya kumekuwa na washindi watano tofauti, huku Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Morocco zikiwa ni mataifa mawili pekee yaliyonyakua mataji mara mbili.

Mashindano haya yalianza rasmi mwaka 2009. Nchi ya DR Cong (Leopards) lilikuwa taifa la kwanza kunyankua taji la CAF CHAN baada ya kuwashinda Black Stars, Ghana katika fainali ya kwanza iliyochezwa Cote d'Ivoire. Zambia ilimaliza wa tatu baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senegal.

Makala ya pili ya mashindano hayo ilifanyika nchini Sudan mwaka 2011, ambapo Tunisia walitawazwa mabingwa kufuatia ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Angola. Huku wenyeji Sudan wakimaliza wa tatu.

Taifa la kaskazini mwa Afrika, Libya lilishinda katika ardhi ya Afrika Kusini mwaka 2014. Ushindi wa Libya ulikuja baada ya ushindi wa mikwaju ya penalti ya 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana dhidi ya Ghana.

Baada ya kunyanyua taji la kwanza, DR Congo walitwaa tena taji la pili nchini Rwanda mwaka 2016. Katika fainali waliishinda Mali kwa ushindi wa 3-0. Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Cote d'Ivoire.

Morocco ndio taifa pekee kushinda shindano hili kama wenyeji baada ya kuandaa CHAN 2018. Fainali ilikuwa nzuri kwa wenyeji ambapo waliwasambaratisha Nigeria 4-0 na kubeba ubingwa katika ardhi ya nyumbani.

Wamorocco pia wakawa taifa la kwanza kushinda mataji mfululizo ya CHAN. Walitete taji lao kwa ushindi wa 2-0 kwenye fainali dhidi ya Mali, katika mashindano yaliyofanyika 2020 huko Cameroon.

Algeria ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya 2022. Fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela nje mjini Algiers. Ilihitimika kwa Senegal kunyakua taji hilo, baada ya mikwaju ya penalti 5-4.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI