Header Ads Widget

DRC NA RWANDA ZAKUTANA KWA MKUTANO WA KWANZA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO YA AMANI

 

Rwanda na DR Congo zilitia saini makubaliano ya amani mjini Washington mwishoni mwa Juni kwa upatanishi wa serikali ya Marekani.

Wawakilishi kutoka serikali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda wamekutana mjini Washington wiki hii kwa mkutano wa kwanza wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa makubaliano ya amani ya nchi hizo yaliyotiwa saini Agosti 27 (6) mwaka huu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema kuwa mkutano wa kwanza ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka serikali ya Marekani, Qatar, Togo (kama mpatanishi wa Umoja wa Afrika), na Tume ya Umoja wa Afrika.

Mkutano huo uliitishwa na jopo la 'Kamati ya Pamoja ya Uangalizi', yenye jukumu la kufuatilia utiifu wa mikataba hii, kupokea malalamiko ya ukiukaji, kuchukua hatua dhidi ya ukiukaji wa mikataba hii, na kutatua migogoro kwa amani.

Makubaliano ya Amani ya Washington yanasema kwamba pande zote mbili zilijitolea kuanzisha jopo hili la pamoja ndani ya siku 30 baada ya kutiwa saini kwake na kufanya kazi "katika kanuni zilizokubaliwa na pande zote".

Makubaliano muhimu yanayofuatiliwa na jopo ni pamoja na:

DRC kuacha kuunga mkono FDLR(wapiganaji wanaoipinga serikali ya Kigali ndani ya DRC ) na vikundi vingine vya waasi

Kuwatafuta na kujua walipo na kuwamaliza wafuasi wa FDLR

Rwanda kuondoa hatua zake za kujilinda

Kuwalinda raia na kuheshimu sheria za kimataifa

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI