Header Ads Widget

NGOMBARE MWIRU WA AAFP ACHUKUA FOMU YA URAIS KUANZA NA UZALENDO

 

Na Hamida Ramadhan, Matukiodaima Media Dodoma

MGOMBEA Urais wa Chama cha  Wakulima (AAFP), Kunje Ngombare Mwiru , amekuwa mgombea wa mwisho kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais leo Agosti 9,2025 huku akitaja kipaumbele cha uzalendo. 

Ngombare Mwiru ambaye amechukua fomu hizo katika Tume Huru ya  Taifa ya Uchaguzi (INEC) anakuwa mgombea wa tatu kuchukua fomu akitanguliwa na Samia Suluhu Hassan na Dkt Emmanuel Nchimbi  (CCM) na Hassan Almas na Ally Hassan wa (NRA) 

Mgombea huyo  aliwasili katika ofisi za INEC majira ya saa 9:19 alasiri akiwa kwenye gari namba  T 439 Nissan Patrol huku wapambe wake wakiwa na Coaster yenye namba za usajili T 649 EHV na  aliambatana  na mgombea mwenza, Chumu Abdallah Juma na alikamilisha zoezi hilo saa 9:57 jioni.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, mgombea huyo alitoa salamu za pole kwa Watanzania kufuatia kifo cha kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Job Ndugai, akisema kuwa taifa limepoteza mzalendo na kiongozi aliyekuwa na mchango mkubwa katika uongozi wa nchi.

Aidha, Ngombare Mwiru ameipongeza INEC kwa maandalizi bora ya mchakato wa uchaguzi, akibainisha kuwa mazingira yaliyoandaliwa ni ya haki na yanayompa matumaini kuhusu demokrasia ya kweli.

"Mchakato umeandaliwa kwa weledi, tunapongeza INEC kwa kuhakikisha kila mgombea anapata nafasi ya haki," alisema.

Mgombea huyo ameeleza kuwa vipaumbele vyake vitatu vikuu ni "uzalendo, uzakendo, na uzalendo", akisisitiza kuwa taifa linahitaji viongozi wanaoweka mbele maslahi ya nchi kabla ya maslahi binafsi.

Ngombare Mwiru  anatarajiwa kuanza kampeni zake kwa kutembelea mikoa 10 katika harakati za kusaka wadhamini na kuzungumza na wananchi kuhusu dira yake ya uongozi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI