Header Ads Widget

RC BABU NA KIHONGOSIATOA RAI KWA WANANCHI KANDA YA KASKAZINI KUTUMIA MAONESHO YA NANENANE KUJIFUNZA TEKNOLOJIA ..

 



Na,Jusline Marco:Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema Kanda ya Kaskazini ina fursa nyingi za kuendeleza kilimo na ufugaji ambazo zitasaidia kutoa ajira kwa vijana wasiokuwa na ajira kupitia matumizi bora ya maeneo ya kilimo yaliyopo.


Babu ametoa kauli hiyo Agust 8 mwaka huu kwenye kilele cha maadhimisho ya 31 ya kilimo na sherehe za nanenane 2025 kanda ya kaskazini yaliyofanyika Kikanda katika Mkoa wa Arusha.



Aidha amesema kuwa sekta ya mifugo imepiga hatua kubwa yenye tija ambapo amewataka wananchi kuendelea kutembelea mabanda yaliyomo ndani ya viwanja hivyo vya Them Njiro Mkoani humo ili kujionea teknolojia na maarifa yanayoboresha shughuli za ufugaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenani Kihongosi amesema kuwa serikali imeendelea kutoa fedha nyingi kwa wizara ya kilimo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wakulima wananufaika na miradi ya maendeleo ikiwemo afya,miundombinu ya barabara,viwanda na biashara hatua ambayo inalenga kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.


Ameongeza kwa kutoa wito kwa wananchi kusimama imara katika kulinda na kutunza amani ya Mikoa ya Kanda ya Kaskazini na Tanzania kwa Ujumla, sambamba na kujiepusha na wanaohamasisha vurugu kwani amani iliyopo nchini ndiyo msingi wa maendeleo makubwa yanayoshuhudiwa chini ya serikali ya awamu ya sita.


Kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu 2025 ni Chagua viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya kilimo mifugo na uvuvi 2025

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI