Header Ads Widget

WAJUMBE 2 WA VUGUVUGU LINALOJIITA "FBI" KENYA MAHAKAMANI WAHUSISHWA NA UGAIDI

 


Maafisa wa upelelezi wamemkamata na kumfikisha mahakamani Patrick Nyambaka Osoi, mwanachama mwanzilishi wa vuguvugu la Kupambana na Ukatili na Kutoadhibi makosa (FBI), wakati wa operesheni iliyoratibiwa vyema kando ya Barabara ya Lang'ata jijini Nairobi.

Taarifa ya Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya (DCI) inasema, Osoi alikabiliwa na mashtaka chini ya sheria ya kuzuia Ugaidi, ya mwaka 2012, na kwa kuwa na bunduki, miongoni mwa makosa mengine.

Kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthaiga jijini Nairobi huku akisubiri uamuzi wa mahakama juu ya amri za kizuizi zilizopangwa kufanyika Alhamisi.

Katika tukio jingine, Jackson Kuria Kihara, almaarufu Cop Shakur, pia alikamatwa katika kitongoji cha Kahawa West kuhusiana na makosa hayo hayo. Wakati wa kukamatwa, alipatikana akiwa na kofia nyekunduyenye alama ya 'FBI'.

Kihara atafikishwa mahakamani anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Kahawa leo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI