NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA
WABUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve na Nancy Nyalusi wamefanikiwa kutetea nafasi zao kwa kushinda kwa kishindo kura za maoni.
Akitangaza matokeo hayo Jana msimamizi wa uchaguzi huo Kheri James alisema kuwa Rose Tweve ameongoza kwa kwa kupata kura 554 huku Nancy Nyalusi akifuatia kwa kura 507 na mhandisi Fatma Rembo akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura
326 .
Nafasi ya Nne ikishikwa na Seki Kasuga aliyepata kura 152 na mwahabari Tumain Msowoya akipata kura 31.
Huku Maria Makombe akipata kura 59 Libya Nzema Kura 25 ,Scola Mbosa akipata kura 8.
Wakishukuru baada ya uchaguzi huo Rose Tweve alisema kuwa anapongeza wajumbe kwa kumwamini na kuwa haya ni matokeo ya wajumbe na anasubiri maamuzi ya vikao vya juu huku akiahidi kuendeleza ushirikiano na wajumbe .
0 Comments