NA MATUKIO DAIMA MEDIA
IRINGA.
WANACHAMA 6 wa chama cha mapinduzi walioteuliwa kupita katika mchakato wa kura za maoni kati ya 17 waliochukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo hilo leo wamejinadi kuomba kupigiwa kura za maoni.
Wanachama wanaowania nafasi hiyo kupitia CCM katika hatua ya kura za maoni kwa wajumbe ni pamoja na Jesca Msambavangu ,Fadhili Ngajilo, Wakili Moses Ambindwile, Mchungaji Peter Simon Msigwa, Islam Huwel, na Nguvu Chengula.
Akizungumza na wajumbe mwanachama Mchungaji Peter Msigwa ameomba kura kwa wajumbe katika kata ya Mivinjeni Manispaa ya Iringa ili kuweza kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu.
Akijieleza na kuomba kura mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM kata ya Mshindo Mch Msigwa na wabunge wengine watano walioteuliwa wameomba kura za ndiyo kutoka kwa wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Mivinjeni, na mshindo.
Msigwa alisema kuwa wakati yupo Mbunge kupitia chama pinzani alifanya mambo mazuri hasa katika ujenzi wa miundombinu, afya na kuahidi kuwa kwa sasa yupo chama tawala atafanya mambo makubwa zaidi kwa kushirikiana na viongozi walioko madarakani .
"Zamani nilikuwa chama cha mama wa kambo ila kwa sasa nimerudi CCM hivyo naombeni kura zenu ili nikawasemee wananchi wa iringa katika shughuli za maendeleo, nitahakikisha nakomesha mikopo umiza kwa kuwasaidia akina mama kupata mikopo ya ya halmashauri na mfuko wa jimbo"alisema
kwa upande wake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu, amesema iwapo watampa ridhaa hiyo, atahakikisha anakwenda kukamilisha miradi yote ya maendeleo ambayo aliaanzisha awali pamoja na kuibua mingine mpya.
"Katika jimbo hili tunamaono kuwa liwe jimbo la kitalii ambalo litafanana na kitalii, tumeanza kuweka lami katika baadhi ya barabara ili kupunguza msongamano ya magari makubwa katikati ya mji,pamoja na kuwapa vibali kwa ajili ya ukarabati wa nyumba zilizopo katikati ya mji na uchimbaji wa visima"alisema
Wagombea hao wameendelea kujinadi mbele ya wajumbe wa kata mbalimbali, wakieleza dhamira na mipango yao ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Iringa Mjini, endapo watapewa nafasi ya kuiwakilisha CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Naye Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Fadhili Ngajilo, ameomba kura za ndiyo kutoka kwa wajumbe wa Kata ya Mivinjeni na Mshindo ili kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini.
Ngajilo, am
baye awali alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Iringa kabla ya kujiuzulu nafasi hiyo kwa ajili ya kugombea ubunge, amesema ameomba ridhaa ya wajumbe hao kwa mara nyingine kutokana na nia yake ya dhati na wito wa kuwahudumia wananchi wa Iringa.
“Nilijiuzulu nafasi ya uongozi kwa heshima ili niweze kugombea ubunge, si kwa sababu ya tamaa ya madaraka, bali kwa sababu ya wito na mapenzi niliyonayo kwa wananchi wa Iringa.
Ninaamini nina uwezo, uzoefu na maono ya kuwatumikia kwa ufanisi,” alisema Ngajilo mbele ya wajumbe hao.
Mteule mwingine Wakili Moses Ambindwile ambaye ni mwanasheria kwa taaluma, amesema endapo atapewa ridhaa hiyo na baadaye kuchaguliwa kuwa mbunge, ataweka kipaumbele katika kuwahudumia wananchi wa Iringa Mjini kwa kutoa msaada wa kisheria bila malipo kupitia ofisi yake ya sheria.
"Najua changamoto nyingi zinazowakabili wananchi, hasa katika masuala ya sheria, mikataba, migogoro ya ardhi na familia.
Ameahidi kutoa elimu ya uwekezaji, fedha na uchumi kwa wananchi, ili kuwawezesha kuondokana na hali ngumu ya maisha, na hasa kuwaepusha na mikopo kandamizi inayojulikana kama “kausha damu” ambayo imekuwa kikwazo kwa wanawake wengi kwa sababu ya kukosa elimu ya kifedha.
kwa upande wa Nguvu Chengula alisema kuwa anaomba kura za ndio ili aweze kuwakilisha bungeni kwa kuwa nia anayo,uwezo anao na nguvu pia anazo.
"Leo nimekuja kwenu kwa heshima kubwa muwezze kunihurumia mtoto wa mwenzenu mnipe nafasi ya kuwawakilisha bungeni, katika karatasi ya kupigi kura mimi nitakuwa namba mbili, ni mtu wa pili katika karatasi hiyo"alisema
"Nipeni nafasi ya kuwatumikia mwaka 2020 mlisema nisubiri kidogo, na huu ndio wakati mwingine nimerudi na sikukata tamaa niliendelea kuwa na CCM na CCM hii ndio imenichakaza kama mnavyoniona na naelekea kuwa masikini naombeni kura zenu nipate nafasi niweze kuambulia japo matone msiniache wana mshindo nikaaibika"alisema
0 Comments