Na Gift Mingi
Moshi
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amezindua rasmi kampeni ya twende zetu kileleni awamu ya tano lengo likiwa ni kuhamasiha utalii wa ndani.
Kampeni hiyo imekuwa ikiratibiwa na kampuni ya Zara Adventure kwa kushirikiana na hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)pamoja na shirika la hifadhi za taifa (TANAPA).
Babu amesema kampuni hiyo imekuwa ikiratibu kampeni hiyo ambapo kwa mwaka huu litafanyika mwezi desemba mwaka huu.
Alisema jitihada hizo ni kuunga mkono kampeni ya kuutangaza utalii uliokoasisiwa na rais dkt Samia Suluhusu Hassan kupitia filamu ya The royal Tour
Alisema kupitia filamu hiyo watalii wameongezeka tofauti na miaka mingine na kukuza pato la taifa kwa ujumla.
0 Comments