Header Ads Widget

TAASISI YA MAMA KIJANI YATUA SINGIDA,YAAHIDI KUMPAMBANIA RAIS SAMIA

 

Na Thobias Mwanakatwe, 

Taasisi ya Mama Kijani inayoundwa na wanawake wafanyabiashara imezinduliwa rasmi katika Mkoa wa Singida lengo ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambapo inatarajia kusajili zaidi ya akina mama 500.

Mwenyekiti  wa Taifa wa taasisi hiyo, Magreth Songay, akizungumza jana alisema Taasisi ya Mama Kijani inaendeshwa katika mikoa yote nchini lengo kuu ni kumuunga mkono na kutangaza kazi zote nzuri zinazofanywa na serikali chini ya Rais Samia.

"Mama Samia amefanya kazi nzuri sana katika nchi yetu kila mkoa kuna miradi ya mabilioni ya fedha imetekelezwa kwa hiyo taasisi hii katika kila mkoa itakuwa inatangaza maendeleo yaliyofanywa na serikali kwa wananchi," alisema Songay. 


Songay alisema taasisi hiyo itakuwa inatembelea miradi yote iliyotekelezwa katika mikoa na kuitangaza kwa wananchi ili waweze kufahamu kazi zilizofanywa na serikali kwa lengo la kumuunga mkono  rais Dk.Samia Suluhu Hassan hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

"Nchi yeti ilikuwa na changamoto la vifo vya wanawake wajawazi na watoto, ukosefu wa maji lakini tangu Rais Samia aingie madarakani changamoto hizo zimetatuliwa na hivyo tunaona mama yetu huyu anapaswa kuungwa mkono ili aendelee kupata nguvu za kuifanya vyema kazi za kuleta maendeleo nchini," alisema Songay.

Aidha, Songay alitoa wito kwa wanawake wote nchini kuendelea kuhamaisha pamojana na kuwashawishi waume zao,marafiki,ndugu na  jamaa waendelee kumuunga mkono Rais Samia ili itakapofika Oktoba mwaka huu iwe rahisi wakati wa uchaguzi.

Naye Mwenyekiti wa taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Jackline Peter, alisema wanawake wa Mkoa wa Singida wameipokea Taasisi ya Mama Kijani kwa mikono miwili na hivyo watahakikisha wanafanyakazi usiku na mchana kumsapoti Rais Samia.


Peter alisema wanawake hawana budi kumuunga mkono rais Samia kwani amefanya mambo mengi ya maendeleo katika kipindi kifupi cha utawala wake jambo ambalo limewaheshimisha wanawake nchini kwamba wakipewa nafasi wanaweza.

Kwaupande wake Katibu wa Taasisi ya Mama Kijani Mkoa wa Singida, Jackline Omary alisema taasisi hiyo inatarajia kusajili zaidi ya wanawake 500 ambapo katika siku ya kwanza ya uzinduzi wanawake 50 wamesajiliwa na kupewa kadi za chama.

Omary alitoa wito kwa wanawake wa Mkoa wa Singida kujirikeza kwa wingi kujiunga katika taasisi hiyo ambayo pia mbali na kuunga mkono kazi zinazofanywa na serikali lakini pia inasaidia kuwainua kiuchumi wanawake.

















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI