Header Ads Widget

SERIKALI YAPONGEZWA KUUNGANISHA NGUVU NA WADAU KUWAPIGANIA WASICHANA KUFIKIA MALENGO YAO


 Mwenyekiti wa GPE Duniani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete ameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada na hatua ilizofikia katika elimu kwa kuwezesha watoto wengi kuendelea na masomo, kuongeza ufaulu ngazi za sekondari ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu.

Mhe. Kikwete aliyasema hayo Kibasila sekondari Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kumkaribisha Mwanzilishi wa Mfuko wa Malala (Malala Fund) aliyekuja kwa mwaliko wa Kiongozi huyo. Kikwete amemtaja Malala kama shujaa wa kumpigania mtoto wa kike hususani wakati huu wa Sayansi na Teknolojia ambayo haitakiwi kumwacha nyuma mtoto yeyote.

Aidha, alisema Mfuko wa Elimu Duniani GPE umewezesha kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji wa wanafunzi na walimu kwa kujenga miundombinu ya madarasa 2980, vituo vya walimu (TRC) 252, uchapaji wa vitabu 36118000, matundu ya vyoo 7673, nyumba za walimu 64 na shule mpya 18 ambazo zimechangia kuleta mabadiliko nchini 


Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. QS Kipanga, alisema kuwa maboresho ya mitaala nchini yanalenga kuwahakikishia wanafunzi wote, hususan wasichana na wale wenye mahitaji maalum, mazingira salama na jumuishi ya kujifunzia yanayowasaidia kufanikisha malengo yao ikiwepo matumizi ya teknolojia za kidijitali, ikiwemo Akili Mnemba (AI) na TEHAMA

Vilevile, Mhe. Kipanga alisisitiza kuwa Serikali inaamini kuwa kumuelimisha mtoto wa kike ni njia ya msingi ya kulitendea haki Taifa kwa kulikomboa kiuchumi na kijamii lakini pia hadi sasa wanafunzi wapatao 13,272, wengi wao wakiwa wasichana, wamepata fursa ya pili ya kuendelea na elimu ya sekondari kupitia vituo vya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (IAE).

Bi. Malala Yousafzai, Mwanzilishi wa Mfuko wa Malala (Malala Fund), alisherehekea siku yake ya kuzaliwa tarehe 12 Julai, 2025, Wilayani Kongwa, Tanzania akieleza kufurahishwa na mazingira mazuri yanayoandaliwa kuwawezesha watoto wa Kitanzania kupata elimu. Malala alitoa wito kwa jamii na wadau kuungana kuwasaidia wasichana kutoka katika mazingira na historia tofauti ili wafikie ndoto zao. 


Joyline Buntu, mwanafunzi wa Kidato cha Pili kutoka Shule ya Sekondari Kibasila, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Programu ya GPE na Taasisi ya Jakaya Kikwete kwa kuunganisha nguvu pamoja na kuwezesha wanafunzi kama yeye kubaki shuleni, kujifunza kwa ufanisi, pia kujenga miundombinu bora na kufikia ndoto zao bila kukumbana na vikwazo vyovyote.

Malala Yousafzai, Mwanzilishi wa mfuko wa Malala alitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kujionea moja ya Taasisi ambayo inatekeleza jukumu la kuwainua wasichana waliorudi shule baada ya kuanguka (school dropout) la ‘Msichana Initive’ lakini pia kuunga mkono jitihada za kuwawezesha wasichana nchini ambapo anatarajiwa kuwekeza kiasi cha shilingi Bilioni 8 mwaka 2026.





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI