Header Ads Widget

NONDO AMVAA ZITTO UBUNGE KIGOMA MJINI

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mwenyekiti wa Taifa wa  ngome ya vijana wa Chama cha ACT Wazalendo Abdul Nondo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kumteua kuwa mgombea ubunge wa ACT Wazalendo katika jimbo la Kigoma Mjini.

Nondo alichukua fomu  katika ofisi za ACT Wazalendo jimbo la Kigoma Mjini Ujiji mjini Kigoma ambapo alisema kuwa amechukua fomu akiomba ridhaa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo katiia uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Mwenyekiti huyo wa ngome ya vijana alisema kuwa amechukua fomu ikiwa ni kufuata matakwa ya katiba ya nchi na kutimizi misingi ya demokrasia ambayo inaruhusu mwanachama wa chama cha siasa mwenye sifa kugombea nafasi za uwakilishi wa wananchi na kwamba binafsi amejipima na kuona anatosha kwenye nafasi hiyo.

Kuchukua fomu kwa Abdul Nondo kunafanya hadi sasa wanachama wawili kuwa wamechukua fomu katika jimbo hilo akiwa anatarajia kuchuana na Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye alionesha nia na kuchukua fomu kuomba ridhaa cha chama hicho kumteua kuwa mgombea ubunge jimbo la Kigoma Mjini.

Mwenyekiti huyo wa vijana amemzungumzia  aliyewahi kuwa Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini manispaa ya Kigoma Ujiji kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Clayton Revocatus Maarufu Baba Levo ambaye amechukua fomu kupitia CCM kuomba kugombea jimbo hilo kwamba hata CCM wakimpitisha hataweza kupambana na mgombea wa ACT Wazalendo na kushinda.

Katibu wa ACT Wazalendo jimbo la Kigoma Mjini,Iddi Adam akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama hicho alisema kuwa hadi sasa wanachama wawili wamechukua fomu kuomba ridhaa ya chama hicho kuteua mmoja wao kugombea ubunge kwa jimbo la Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo.

Adam alisema kuwa Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe alichukua fomu Tareh nne  mwezi Mei mwaka huu  hivyo hadi sasa ni wanachama hao na zoezi la nddani ya chama kuchukua na kurudisha fomu linatarajia kuhitimishwa Julai 15 mwaka huu ili kuruhusu upigaji kura za maoni kupata mgombea.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI