Header Ads Widget

INEC YAWATAKA WARATIBU,WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUZINGATIA MAELEKEZO, KUACHA MAZOEA

 

Na Lilian Kasenene, Morogoro

Matukio DaimaApp 

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi,maafisa uchaguzi na ununuzi kuzingatia maelekezo watakayopewa na tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jaji wa mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele alisema hayo mjini Morogoro,wakati wa mafunzo ya siku tatu yanayohusisha waratibu wa uchaguzi,wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa ichaguzi ngazi ya jimbo, maafisa uchaguzi, maafisa ununuzi na maafisa TEHAMA kutoka mikoa ya Dodoma,Morogoro na Singida.

Jaji Mwambegele alisema pamoja na baadhi yao kuwa na uzoefu katika uendeshaji wa Uchaguzi, baadhi ya mambo kumekuwa na mabadiliko makubwa ya sheria katika uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka huu.


"Mabadiliko kama hayo utofauti wa utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi huu na chaguzi zilizopita,wakati wote wa mchakato wa uchaguzi huu, ni vema mkavishirikisha kwa karibu vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili na wadau wengine wa uchagu katika maeneo yenu,"alisema.

Kuhusu masuala yote muhimu ya kiuchaguzi wanayostahili kushirikishwa Jaji Mwambegele alisema jambo hilo litawarahisishia utekelezaji wa majukumu yao ilimradi hayakinzani na Katiba, sheria, kanuni na maelekezo yaliyopo.

Mwenyekiti huyo wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi alisema ni muhimu kuhakikisha wanayatambua na kuyajua vyema maeneo ambayo uchaguzi utaendeshwa ikiwemo miundombinu ya kufika katika vituo vya kupigia kura.

Pamoja na mambo aliyobainisha alisisitiza masuala ya kufanya utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji maalum ya vituo husikana kuhakikisha kunakuwa na mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani.

Pia akawataka kuhakikisha wanaajiri watendaji wa vituo wenye weledi, wanaojitambua na kuachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi.

Kuhakiki vifaa vya uchaguzi wanavyopokea kutoka Tume na kuhakikisha kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema na kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala.

Aidha aliwataka kuhakikisha siku ya uchaguzi mnaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi kwa mujibu wa sheria ya Tume.

Mkurugenzi wa uchaguzi INEC Ramadhan Kairima alisema jumla ya washiriki 165 kutoka Halmashauri 24 za Mikoa mitatu wanapatiwa mafunzo hayo yenye ujuzi.

Mmoja wa washiriki, msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Mvomero Mery Kayowa alisema wao kama wasimamizi Wana matarajio ya kutekeleza maelekezo na miongozo ya kuwawezesha kusimamia misingi inayotarajiwa ya haki na uhuru chini ya Tume huru ya Taifa ya uchaguzi.

Kayowa alisema imani yao, ushiriki wa kila mdau katika dhana nzima ya Uchaguzi ni haki y msingi na hiyo itaondoa dhana tofauti kwa sababu kila mmoja ana hali ya kushiriki na kutoa maoni yake.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha masuala muhimu kuhusiana na usimamizi, uratibu na uendeshaji wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI