Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio DaimaApp
Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kampasi ya Morogoro imewapatia viakisi(Reflectors)20 waendesha bodaboda lengo likiwa ni kuelimisha umma kuhusu ulinzi na usalama kwa waendesha bodaboda na abiria wanaosafirishwa.
Kaimu Polisi jamii Wilaya ya Morogoro mkaguzi wa Polisi Kasimu Makadi akigawa viakisi hivyo kwa waendesha bodaboda aliwataka kuvitumia kwa usahihi na kwamba hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa uhalifu kwenye eneo hilo.
Makadi alisema TEWW kupitia vituo vyake kwenye mikoa 26 ya Tanzania bara ina jukumu la kusaidia kupunguza tatizo la uhalifu kupitia elimu kwa umma huku aliwataka kubuni program mbalimbali za kusaidia wananchi ambapo waendesha bodaboda ni sehemu ya jamii hiyo.
Naamini mtatumia maarifa na ujuzi kutoka taasisi hii iliyopo katika eneo hili la Forest kujifunza Maadili mwema ili kutekeleza majukumu yenunua usafirishaji watu kwa manufaa ya Taifa letu kwa ujumla,"alisema.
Mkaguzi huyo wa Polisi pia alisema alipongeza taasisi hiyo ya TEWW kwa kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake kwani imekuwa msaada mkubwa kwa watanzania katika kuelimisha kwa kujua kusoma,kuandika na kuhesabu ambapo kimekuwa kisomo chenye manufaa.
Aidha alisema waendesha bodaboda kama sehemu ya jamii inapaswa kuwa nao kwa ukaribu kwani ndio wamekuwa wakitumika kubeba abiria kwenye maeneo mbalimbali hivyo kwa kufanya kazi ya kuwapatia viakisi hivyo itakuwa msaada mkubwa kwa kampasi hiyo kuwa na madereva wanaoaminika ambao watakuwa wakivaa viakisi hivyo.
Akaiomba taasisi hiyo kuendelea kutoa Elimu kwa makundi tofauti kama waendesha bodaboda ili suala la ulinzi na usalama liwe la kila mmoja badala ya Jeshi la Polisi ikizingatiwa kuwa taasisi Sasa imetimiza miaka 50 na huo ni uzoefu wa kutosha kwa kutoa Elimu kwa watu wazima.
Kaimu meneja TEWW kampasi ya Morogoro Ferdinand Byenobi, akizungumza katika uzinduzi huo, alisema katika kuhakikisha taasisi inatoa mchango wake kwenye jamii imeonelea kutoa Elimu ya ulinzi na usalama kwa wasafirishaji wa bodaboda na wasafirishwaji ukiwa ni jukumu mojawapo la TEWW kuhusu kutoa Elimu kwa umma.
Byenobi alisema akawapongeza waendesha bodaboda kwa huduma ya usafirishaji abiria wanazozitoa,huku akiwataka kuvaa wakati wote viakisi walivyopatiwa ili watambulike eneo wanalotoka pindi panapotokea tatizo.
"Pamoja na kutangaza miaka 50 ya Taasisi niwaombe muwe chachu ya kuwa walinzi wa usalama wa abiria na Mali zao katika kuleta Maendeleo ya Taifa letu,niwaase mkawe waadilifu na kuacha vitendo vinavyokiuka maadili mema kama matumizi ya dawa za kulevya na mengine yoyote yanayoathiri utendaji kazi wenu,"alisema.
Mmoja wa abiria wa bodaboda Rose Mwilongo alisema waendesha bodaboda kuwa na reflector itasaidia kuaminika na hata abiria anapotokea amesahau mzigo kwa namna Moja ama nyingine ni lahisi kumtambua, akawakumbusha abiria wenzake wanapopanda pikipiki kikariri namba na eneo alipopandia.
Mwenyekiti wa bodaboda eneo la Wamo forest Clement Joseph alisema wao kama wasafirishaji Wana wajibu wa kumlinda abiria na Mali zake, ambapo aliahidi kuendelea kuwa walinzi wa abiria hao pindi wanapotoa huduma kwako.
0 Comments