Header Ads Widget

MBIO ZA MSAKUZI PANDE GAME RESERVE ZAZINDULIWA RASMI

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga 


Na. Joyce Ndunguru, Dar es Salaam.

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kushirikiana na Msakuzi Sports Promotion leo Julai 12,2025, imezindua rasmi msimu wa kwanza wa  mbio za riadha zinazojulikana kama "Msakuzi Pande Game Reserve Marathon" zilizofanyika katika Hifadhi ya Pande iliyopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga amesema lengo kuu la mbio hizi ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan za kutangaza na kuhamasisha utalii.

"Sote ni mashahidi juhudi hizi zimeweza kuongeza idadi ya watalii wa nje na ndani, ukiangalia idadi ya watalii wa ndani wameongezeka kutoka takribani watalii laki tisa mwaka 2021 hadi watalii takriban Milioni tatu kwa mwaka 2024" amesema Dkt. Lwoga 

Sambamba na hilo, Dkt. Lwoga amesema mbio hizi zimejikita pia katika kuhamasisha jamii kushiriki kwenye michezo ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

"Mbio hizi zina tija sio kwenye michezo pekee ila zinahamasisha utalii na kujenga afya zetu, na hakika zimefanikiwa tumekimbia, tumeburudika, tumeona wanyamapori mbalimbali, unakimbia huku unavuta hewa safi" ameongeza Dkt. Lwoga.


Kwa upande wake, Kamanda wa Hifadhi ya Pande, Dorothea Massawe amesema mbio za Msakuzi Pande Game Reserve zimejumuisha washiriki takribani 300 na zimeambatana na shughuli zingine za utalii kama vile mlo wa porini (nyamapori choma) na kuona wanyamapori mbalimbali wanaopatikana katika Hifadhi hiyo wakiwemo Simba, Chui, Pundamilia, Mbuni, Kasongo na pundamilia.

Naye, Katibu wa Msakuzi Sports Promotion, Peter Mpulila ameushukuru uongozi wa TAWA kwa ushirikiano walioupata hadi kukamilika kwa mbio hizo.

Kadhalika, Bw. Mpulila ameongeza kwa mbio hizi zimejikita katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza na kutangaza vivutio vya utalii vilivyo ndani ya nchi.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI