Header Ads Widget

MAANDALIZI YA MAPOKEZI YA RAIS DKT SAMIA KWA UZINDUZI WA BANDARI KAVU KWALA MKOANI PWANI YAMEKAMILIKA - RC KUNENGE


 MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge  amesema maandalizi ya uzinduzi wa Bandari Kavu ya Kwala unaotarajia kufanywa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan Julai 31,2025 yanaendelea vizuri.

Kunenge ,ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Julai 30,2025 mara baada ya kukagua maandalizi ya uzinduzi huo katika maeneo yote muhimu.

Amesema ,Mkoa umejipanga vizuri katika kupokea ugeni huo ambapo amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali ombi la kuwa mgeni rasmi pamoja na kuwa ngumu..

Kunenge ,amesema kuwa Rais Samia akiwa katika eneo la Kwala atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo  kuzindua safari rasmi safari  ya treni ya Mwendokasi (SGR) ya kubeba Makasha na kuzindua bandari Kavu ya Kwala .

Amesema Rais pia ataweka jiwe la msingi katika Kongani ya viwanda itakayokuwa na viwanda 250 ambapo mpaka sasa tayari viwanda saba vimekamilika na vingine vinne vipo katika hatua ya ujenzi.

Kunenge amesema bandari Kavu ya Kwala itaongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam ambapo kimsingi bandari Kavu hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa Makasha katika bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 30.

Amesema eneo la Bandari Kavu ya Kwala itaileta nchi za Afrika pamoja zaidi ya 11 na kwamba mpaka sasa nchi tisa tayari  zimeanza mchakato wa kujenga bandari Kavu kwa ajili ya nchi zao ambapo ametaja nchi hizo kuwa ni 
 Kongo, Zambia,Burundi,Malawi, Zimbabwe na Uganda ambapo pia alisema Sudan na Somalia nao wameonyesha nia .

Amesema Bandari hiyo itakuwa sehemu ya kuongeza uchumi kwa Wakazi wa maeneo ya Mkoa wa Pwani wanaopitiwa na barabara ya Bandari Kavu na pia itakuwa sehemu ya kuongeza ajira kwa vijana.

Kunenge amewaalika Wananchi wa Mkoa wa Pwani pamoja na maeneo mengine ya karibu kujitokeza kwa wingi kushiriki uzinduzi huo kwa.kumpokea Rais Samia katika ziara hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI