Yoweri Museveni ni mmoja wa marais waliokaa madarakani muda mrefu barani Afrika
Wanachama 15 wa chama cha upinzani cha National Unity Platform nchini Uganda, wameshtakiwa kwa kuharibu mabango ya kampeni ya Rais Yoweri Museveni, kwa mujibu wa ripoti ya tovuti ya kibinafsi ya Chimp.
Polisi wanasema 15 hao waliharibu mabango katika mji mkuu wa Kampala siku chache kabla ya ziara rais katika eneo hilo.
"Washukiwa wanashtakiwa chini ya Kifungu cha 78(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Urais, ambayo inaharamisha upotoshaji wa matangazo na nyenzo za kampeni," Chimp Reports alisema.
Washukiwa hao wanazuiliwa katika gereza la Luzira na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 29 Julai.
Kukamatwa kwa watu hao kunakuja huku joto la kisiasa likipanda baada ya Museveni kuteuliwa tarehe 5 Julai kama mgombea wa chama tawala cha National Resistance Movement katika uchaguzi wa rais wa Januari ujao.
Iwapo atachaguliwa tena, Museveni, 80, ambaye aliingia mamlaka mwaka 1986, anaweza kuendeleza utawala wake hadi takriban miaka 50.
0 Comments