Header Ads Widget

HIZI NDIO FURSA DIRA YA MAENDELEO YA 2050

NA MATUKIO DAIMA APP.

DODOMA.

 Dira ni nini? Dira ni mwongozo au taa ya kutuonyesha ni nini cha kufanya kwa mahali gani, kwa jinsi gani, kwa wakati gani na kwa watu gani.

Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025-2050 imejengwa juu ya msingi mkuu wa utawala bora, amani, usalama na utulivu. Msingi huu unajumuisha hatua muhimu za kuheshimu Katiba, utawala wa kidemokrasia, mgawanyo wa madaraka na utamaduni wa kisiasa unaokuza ushirikishwaji na umoja wa kitaifa.

Katika kutekeleza na kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Dira imeanisha sekta zenye uwezo mkubwa wa kuleta mageuzi ya haraka ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Hizi baadhi ya sekta zenye Fursa za Mageuzi kuelekea 2025-2050, sekta hizi zimebainishwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuchochea kufikiwa kwa malengo ya Dira 2050.

1. Sekta ya Kilimo (uvuvi, mifugo na misitu

Sekta hii bado ni mhimili wa uchumi wa Tanzania, ikichangia asilimia 26.5 ya pato la Taifa, ikiajiri asilimia 65 ya nguvukazi, na kuzalisha asilimia 30 ya mapato ya mauzo ya nje, na ina uwezo wa kuzalisha ajira nyingi na kuchochea ongezeko la mapato kupitia mauzo ya bidhaa zilizoongezwa thamani.

2. Utalii - Sekta hii inachangia asilimia 25 ya mapato ya mauzo ya nje ya Tanzania, ni mojawapo ya sekta kuu za Uchumi. Hivi karibuni sekta hii imekuwa kuwa chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni, ukichochea sekta muhimu kama vile za ukarimu, usafiri na biashara.

3. Sekta ya viwanda - Kwa sasa sekta ya viwanda inachangia asilimia 8.1 ya pato la Taifa na inakua kwa asilimia 8 kwa mwaka. Hivyo, ina uwezo mkubwa wa kuwa na taathira chanya katika sekta nyingine kama vile usindikaji wa mazao na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi. Hii itaongeza thamani ya ndani, itapunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje na kuboresha uzalishaji wa mauzo ya nje.

Kwa kuwa Dira ina lenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha viwanda chenye ushindani kimataifa ifikapo mwaka 2050, basi sekta hii imepewa kipaumbele.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI