Header Ads Widget

CHINA YAMUONYA TRUMP JUU YA USHURU, YATISHIA KULIPIZA KISASI

Bendera ya China na Marekani

China umeuonya utawala wa Trump siku ya Jumanne dhidi ya kuzidisha mvutano wa kibiashara ikiwa itarejesha ushuru kwa bidhaa zake mwezi ujao, na kutishia kulipiza kisasi dhidi ya mataifa ambayo yanaingia mikataba na Marekani ili kuiondoa China katika minyororo ya usambazaji.

Washington na Beijing zilikubaliana juu ya mfumo wa biashara mwezi Juni ambao ulileta mapatano dhaifu, lakini mambo mengi bado hayajapatiwa suluhu.

Msimamo wa China umeelezwa katika makala iliyochapishwa katika gazeti la serikali la People’s Daily, na kusainiwa “Zhong Sheng ama Sauti ya China, kauli inayotumiwa na gazeti hilo kuelezea maoni ya China juu ya sera za nje.

Siku ya Jumatatu, Rais Donald Trump alianza kuwajulisha washirika wake wa kibiashara juu ya ushuru wa juu kutoka Marekani kuanzia Agosti 1, baada ya kucheleweshwa ili kuwapa muda wa kufanya makubaliano ya kiuchumi na Marekani.

China ambayo hapo awali iliwekewa ushuru unaozidi 100%, ina hadi Agosti 12 kufikia makubaliano na Ikulu ya White ili kumzuia Trump kuongeza ushuru zaidi.

Wastani wa ushuru wa Marekani kwa mauzo ya nje ya China kwa sasa ni 51.1%, wakati wastani wa ushuru wa China kwa bidhaa za Marekani ni 32.6%, imesema Taasisi ya Peterson inayofuatilia Uchumi wa Kimataifa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, makala hiyo pia imezungumzia uchumi wa kikanda kwa nchi ambazo zinaingia mikataba na Marekani ya kupunguziwa ushuru na kuiondoa China katika minyororo yao ya usambazaji.

Wiki iliyopita, Vietnam ilipata punguzo la ushuru 20% kutoka 46% kutoka Marekani kwa bidhaa ambazo kwa kawaida hutoka China.

"China inapinga nchi yoyote kuingia makubaliano ambayo yanaathiri maslahi ya China ili kupata makubaliano ya kupunguziwa ushuru," makala hiyo imesema.

"Iwapo hali hiyo itatokea, China haitakubali na itajibu ili kulinda maslahi yake halali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI