Header Ads Widget

CHANJO YA MIFUGO NGORONGORO YAZINDULIWA.

 


Na,Jusline Marco;Arusha

Kiasi cha shilingi billioni 216 zimetengwa kwaajili ya itekelezaji wa zoezi la CHANJO ya mifugo ikiwa ni mpango wa kitaifa wa miaka mitano kuanzia 2025 Hadi 2030 ambapo shilingi billioni 62 tayari zimeshatolewa.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameeleza hayo wakati amezindua zoezi la Chanjo ya Mifugo katika Kijiji cha Mokilal Tarafa ya Ngorongoro Mkoani Arusha ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa miaka mitano wa kuchanja mifugo uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 16 Juni, 2025 Bariadi Mkoani Simiyu.

Aidha amesema Serikali imetoa punguzo la bei na kila Ng'ombe ambapo mfugaji anapaswa kuchangia shilingi mia 500 badala ya  shilingi elfu 1000 na Mbuzi na Kondoo wafugaji watachangia shilingi mia 300 pekee badala  ya shilingi mia 500 ambapo mpango huu unalenga kuwasaidia wafugaji.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Benezeth Lutege amesema sababu za kuchanja mifugo hiyo kuwa ni kuongeza thamani mifugo kwenye masoko ya nje,  kujua idadi ya mifugo na wamiliki wake ili kurahisisha upangaji wa maeneo ya malisho ikiwa ni pamoja na kuwasaidia amana katika vyombo vya kifedha kupata mikopo kwa kuwa taarifa za mifugo yao zitakuwa zinatambulika kwenye mifumo ya kielektroniki kupitia alama ya hereni za utambuzi kwa kila mmiliki wa mifugo.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenani Kihongosi ameeleza kuwa Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro na Mkoa wa Arusha kwa ujumla wamekuwa na muitikio mkubwa katika zoezi hilo na wataendelea kuhamasisha wafugaji wote kuchanja mifugo yao ili kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha maisha ya Wananchi.


Sambamba na hayo Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Emmanuel Shangai ameishukuru Serikali kwa kuwasikiliza Wafugaji na kuwapatia chanjo ya mifugo yao na kuwaomba Wananchi wote kujitokeza kuchanja mifugo hiyo ili kuondokana na maradhi mbalimbali,  kuboresha afya na thamani ya mifugo yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI