Na THABIT MADAI, ZANZIBAR
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema kuwa ipo katika hatua za mwisho za kuanzisha chuo cha Ubaharia ambacho kitakidhi viwango vya kimataifa na kuzalisha mabaharia wengi zaidi.
Imesema kuwa, chuo hicho kitaanza rasmi kwa mwaka 2026 huku taratibu zote zikiwa zimekamilika.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya ya Usafiri Baharini Mtumwa Saidi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM 2020/2025.
Amesema, Chuo hicho kitaongozwa kwa vigezo kwa vigezo vya kimataifa ili mabaharia watakao soma chuoni hapo waweze kutambulika kimataifa zaidi.
“Kwa sasa Serikali kupitia mamlaka ya usafiri baharini inashirikiana na Chuo cha Kikuu cha SUZA kuweza kutengeneza mtaala ambao utatumika kufundishia wanafunzi hao,” amesema.
Ameeleza kuwa Mamlaka tayari imeshaanza mchakato wa ununuzi wa vifaa ikiwemo Meli maalum ya kufundishia.
“Nitoe shaka Wananchi kuwa chuo tayari kimeshaanzishwa lakini kwa sasa tupo katika kutekeleza baadhi ya miongozo inayokwenda sambamba na vigezo vya kimataifa,” amefafanua.
“Sisi hatutaki kufikia huko lazima mikataba na miongozi ya kimataifa tuitimize ili kuwa na chuo bora kitakachotambulika kimataifa na kufungua ajira nyingi kwa vijana wetu,” ameongeza.
0 Comments