Rais William Ruto ametoa hakikisho la kuwaunga mkono polisi huku waandamanaji wakitarajiwa kushiriki maandamano ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu vijana walipojitokeza kupinga Mswada wa Fedha 2024.
Ruto alisema polisi wanajukumu la kuhakikisha usalama, kulinda maisha ya Wakenya na kuzuia uharibifu wa mali.
"Kwa polisi wetu wanaume na wanawake, nataka kusema kuwa kama Rais, ninajivunia sana kile ambacho vyombo vyetu vya usalama wamefanya kulinda taifa letu, kulinda mali, na kuruhusu familia zetu kulala kwa amani", Ruto alisema.
"Kila mtu anayehatarisha maisha yake kwa ajili ya taifa hili ninamuunga mkono kikamilifu, na Serikali ya Kenya iko pamoja naye."
"Bila ya amani na usalama, bila utulivu, hatuna taifa," Ruto alisema.
Kiongozi wa nchi aliwataka wananchi na viongozi wote kuheshimu na kuwaunga mkono polisi akisema wanaojaribu kuwahujumu au kuwatisha maafisa wa usalama wanadumaza maendeleo ya nchi.
Ruto aliongeza kuwa wale wanaotaka kudharau au kutishia vyombo vya usalama wanafanya vibaya.
0 Comments