Header Ads Widget

MAANDAMANO KENYA:KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA TANGU MAANDAMANO YA KUPINGA MSWADA WA FEDHA 2024

Mamia ya watu wanatarajiwa kuingia mitaani nchini Kenya asubuhi ya leo kushiriki katika kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024 yalipotokea ambayo yaliongozwa na vijana wanaojulikana kama Gen-Z.

Machafuko hayo yalifikia kiwango cha waandamanaji kuvamia Bunge na msako mkali wa polisi ukafuatia.

Kulingana na waandaaji maandamano ya leo yanafanyika kwa heshima ya wale waliopoteza maisha yao.

Tarehe 25 Juni 2024 ni moja ya siku yenye kusababisha tumbo joto katika historia ya hivi karibuni nchini Kenya.

Kulingana na Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini humo, takriban watu 60 waliuawa katika machafuko ya majuma kadhaa. Familia nyingi zinasema bado zinasubiri haki na uwajibikaji.

Kifo cha mwalimu akiwa chini ya ulinzi wa polisi na tukio la kumfyatulia risasi mchuuzi mwenye umri wa miaka 22 Boniface Kariuki yamechochea hasira ya umma.

Polisi wanasema maafisa waliohusika na matukio hayo mawili wamekamatwa na kushtakiwa lakini waandamanaji wanasema hiyo imekuwa tabia ya polisi ya muda mrefu kukandamiza raia bila uchunguzi kufanywa.

Mkuu wa polisi wa Kenya Douglas Kanja amewasihi raia kudumisha amani na kuepuka maeneo yaliyowekewa zuio kufikiwa.

Wakati huo huo, vikundi vya asasi za kiraia na balozi za kigeni wameitaka serikali ya Kenya kuheshimu haki ya kukusanyika kwa amani na kufanya uchunguzi wa kuaminika kwa madai ya dhuluma zinazotekelezwa na vikosi vya usalama.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI