Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyeregete katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuwajengea mabweni ili kuepukana na adha ya kutembea umbali mrefu (zaidi ya kilometa kumi) kwenda shuleni hali ambayo huwalazimu baadhi yao kukatisha masomo na utoro wa mara kwa mara.
Hayo yameelezwa na wanafunzi wa shule hiyo wakati wa
uzinduzi wa nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Nyelegete wilayani Mbarali kwenye ziara ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera.
Wanafunzi hao wameeleza changamoto ya umbali kutoka kwenye makazi yao hadi shuleni kwamba imekuwa kikwazo kikubwa cha wao kufanikiwa kielimu kwani baadhi yao wamekuwa wakichelewa shuleni na wengine kukatisha masomo kwa kinachodaiwa kuwa wazazi wao wameshindwa kupangisha makazi yalipo karibu na shuleni (mageto).
kutokana na changamoto hiyo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Dkt. Juma Zubery Homera, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kutenga kiasi cha shilingi Milioni mia moja kwa mwaka ujao wa fedha wa 2025/2026 ili kuanza ujenzi wa mabweni ya wasichana na wavulana shuleni hapo ili kuondokana na changamoto inayowakabili wanafunzi, wazazi na walezi wa eneo hilo.
0 Comments