Header Ads Widget

RAIS SAMIA: ‘KATIBA MPYA ITATEKELEZWA MIAKA 5 IJAYO’

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amelihutubia Bunge rasmi Bunge la nchi hiyo na kutoa ahadi mbali mbali.

Bunge hilo linatarajiwa kuvunjwa rasmi tarehe 3 Agosti ili kutoa fursa kwa taifa hilo kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Akihutubia Bunge 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia amesema: “Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu Tume huru ya Taifa ya uchaguzi iliundwa kwa sheria yake yenyewe ili kujibu rai ya muda mrefu ya wadau wa siasa nchini”.

Aliendelea kusema kuwa: “Niseme kuwa Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi itatangaza hivi karibui tarehe ya siku ya uchaguzi, zoezi la uandikishwaji limeshakamilika nchi nzima, Sote tumeshuhudia mwitikio mzuri wa wananchi kujitokeza kwenye vituo vya wapiga kura”

Rais huyo wa Tanzania amesema kuwa kuwa uhuru wa habari na uhuru wa watu kutoa maoni yao umeongezeka, akitoa mfano kuwa majukwaa ya kutoa habari nayo yameongezeka, ’’ Tunathamini na kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari ”, amesema.

Ameongeza kusema kuwa ''Mchakato wa katiba mpya ni miongoni mwa ahadi ambazo zinaonekana katika ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2025/2030''

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI