Na Matukio Daima Media Misri
Utamduni ni jambo muhimu sana kwa hivyo Wanafunzi na Wahitimu wa lugha ya Kiswahili katika Kitivo cha lugha Chuo Kikuu cha Ain Shams hapa Misri wamefanya tamthilia ya kwanza ya Kiswahili nchini Misri chini ya usimamizi Dkt Shimaa Tarek, Mwanagenzi wa lugha ya Kiswahili katika Kitivo hicho.
Tamthilia hiyo inaonesha majaribio ya Wanafunzi kupata kazi nzuri na kufanya juu chini Ili kufikia ndoto zao nchini mwao badala ya kuhama nje.
Pia, tamthilia hii inaonesha sura ya Misri ughaibuni na maisha ya Misri yamekuwaje na inaonesha ustaarabu wa Misri na Utamaduni wake kwa sababu mfululizo wa tamthilia unachanganyika kwa lugha ya kiarabu na lugha ya Kiswahili.
Tamthilia hiyo ina vipindi vinne na timu ya tamthilia hii nao ni:
Mazin Yasser, Yousef Mohamed, Nada Saed, Hager Gamal, Mahmoud El-egezy, Tarek Saed, Alaa Yahia, Rawan Abdel Nabi, Radwa Ahmed, Esraa Abdel Azeem, Loai Adel, Fatma Ebrahim, Hedaya Hisham, Ebrahim El-Saqa, Esraa Ahmed, Habiba El-Sayed, Walaa Mohamed, Nour El-Din, Asmaa Hagag, Nadia Mahmoud, Basmala Hisham, Nadia Mahmoud, Kareem El-eskndr, Mohamed El-Sayed, Malak Mohab, Zyad Sayed, Rahf Mahmoud, Alsayada Tarek, Aisha Ramadan, Mariem Salama, Seraj El-Din, Wafaa Khaled, Khaled Ali, Rahma Rageb, Abdel Rahman Mohamed, Abdel Rahman El-Kateb, Nermeen Khaled, Marwa Gamal, Abd El-Rahman Mohamed, Mohamed Ahmed , Shahd Mohamed El-Sayed.
Dkt. Shimaa Tarek ndiye mwenye fikra ya tamthilia na msimamizi wa tamthilia hii.
Pia, Dkt. Shimaa alisema tutafanya kazi nyingi sana kwa lugha ya Kiswahili nchini Misri na tutachangia kukuza lugha adhimu kama lugha ya Kiswahili ndani ya Misri na Nje.
0 Comments