Header Ads Widget

KAMERA KUDHIBITI AJALI ZA WANYAMA MIKUMI


Hifadhi ya Taifa Mikumi inajipanga kufunga kamera ili kudhibiti madereva wanaoendesha magari kwa kasi kwenye hifadhi hiyo na kugonga wanyama kwa kiasi kikubwa.

Kamera hizo zitafungwa maeneo zinakoanzia barabara za kuingia na kutoka hifadhini upande wa Morogoro na Iringa ili kuwanasa madereva wasiozingatia sheria za barabarani na usalama wa wanyama.

Kamishna Masesa aliyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari Juni 28/2025 kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu hifadhi hiyo,ambapo alisema wastani wa mnyama mmoja anagongwa kila siku sawa na wastani wa Wanyama 500 kila mwaka katika barabara kuu inayopita ndani ya Hifadhi ya Mikumi kuelekea Iringa na Morogoro.


Kamishna Masesa alisema mradi huo amba unatarajia kugharimu takriban shilingi bilioni 2 za Tanzania  una walenga madereva wasiozingatia sheria pamoja na  utupaji taka hifadhini.

“Tayari upembuzi yakinifu umefanywa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP), tunasubiri fedha ipatikane ili kutekeleza mradi huo eneo la kilometa 50 inayokatiza barabara kuu hifadhini.

“Hatua hiyo ina lengo la kuondoa tatizo la wanyama kugongwa na magari na baadhi ya madereva hukimbia au hata kutelekeza magari yao kwa kuhofia faini.

Aidha katika kipindi hiki ambacho kamera hazijafungwa, Kamishna Masesa alisema, wameanza kufanya doria ili kuwabaini wanaogonga wanyama hususan nyani ambao husogea karibu kuvizia vyakula vinavyotupwa na watumiaji wa barabara hizo.

Kwa mujibu wa seria, mtu anayemgonga twiga na tembo inafikia Dola za Marekani 20,000 sawa na zaidi ya Shilingi milioni 50.


“Anayegonga mnyama tukimkamata lazima alipe faini, hii, inategemea amemgonga mnyama gani. Wapo tuliowakamata na magari yao, wengine wameshindwa kulipa faini na kuyatelekeza”alisema  Kamishna Masesa

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa hifadhi ya Mikumi aliishukuru Serikali kupitia bajeti ya 2025/2026 kwa kuziachia hifadhi za Taifa asilimia 51 ya makusanyo yake ili ziweze kujiendesha katika shughuli za maendeleo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI