Header Ads Widget

KADA WA CCM COMRADE JAPHARI SAIDI APENDEKEZA MAREKEBISHO ZAIDI KATIKA MFUMO WA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA


Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Comrade Japhari Saidi, amepongeza mabadiliko muhimu yaliyofanywa na chama katika mfumo wa uteuzi wa wagombea, akisema kuwa ni hatua inayodhihirisha dhamira njema ya viongozi wa CCM kuhakikisha taifa linapata viongozi wenye uwezo, maadili, na wanaokubalika kwa wananchi.

Comrade Japhari amesema kuwa uamuzi wa kuongeza idadi ya wapiga kura ndani ya mchakato wa uteuzi ni hatua ya kihistoria inayosaidia kupunguza ushawishi wa rushwa na kuongeza uwazi na haki katika uchaguzi wa ndani ya chama. 

“Ni hatua inayoimarisha misingi ya demokrasia na kuleta matumaini mapya kwa wanachama wa kawaida,” ameeleza.

Hata hivyo, ili  hatua hiyo ilete matokeo yanayokusudiwa, Comrade Japhari amependekeza kufanyika kwa marekebisho mengine madogo katika mfumo huo. Pendekezo lake ni kwamba badala ya kupigiwa kura kwa majina matatu tu yanayopitishwa kutoka juu, wanachama wote waliojaza fomu kuomba kuteuliwa kugombea waruhusiwe kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano husika.

“Kwa kuruhusu majina yote ya wagombea waliowasilisha nia kupigiwa kura, tutakuwa tumeongeza ushirikishwaji wa wanachama, kukuza ushindani wa haki, na kuwapata viongozi wanaouzika na kukubalika kwa wananchi kwa sababu ya sifa zao halisi,” amesema.

Comrade Japhari ameongeza kuwa marekebisho hayo yataongeza uhalali wa wagombea wanaopitishwa, na kuongeza imani ya wanachama kwa uongozi wa chama chao, jambo ambalo ni muhimu katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

Mkutano Mkuu wa CCM unatarajiwa kufanyika wiki ijayo moja ya agenda ikiwa ni marekebisho ya Katiba.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI