Header Ads Widget

MFANYABIASHARA ISLAM HUWEL ACHUKUA FOMU YA KUTIA NIA UBUNGE IRINGA MJINI, ASIFU KAZI MAENDELEO MAKUBWA CHINI YA RAIS DKT SAMIA ASEMA NI USHINDI TOSHA

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, IRINGA

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Islam Huwel, ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025. 

Hatua hiyo imezidi kuchochea moto wa kisiasa katika jimbo hilo ambalo limekuwa na ushindani mkubwa wa kisiasa katika chaguzi zilizopita.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Huwel alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kutafakari kwa kina, kusikiliza maoni ya wananchi wa Iringa Mjini na kujipima uwezo wake katika kuchangia maendeleo ya jimbo hilo. 

Alisema amejitathmini na kuona kuwa sasa ni muda muafaka kwake kuwania nafasi hiyo ili kuwatumikia wananchi wa Iringa kwa ufanisi, ikiwa atapata ridhaa ya chama chake na baadaye wananchi.

"Nimeamua kwa dhati kuchukua fomu hii kwa sababu nimejipima na kuona kuwa ninaweza kuwatumikia wananchi wa Iringa Mjini kwa weledi, uadilifu na kujituma.

Hata hivyo alisema kwa kuwa ametia nia tu anasubiri muda ukifika wa chama kuruhusu kusema nini atafanya hapo atazungumza zaidi .

Hata hivyo alisema kuwa kazi nzuri zinazofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni nguvu tosha ya ushindi kwa CCM .

 Huwel  pia alisifu kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia , akisema kuwa mafanikio hayo ni kichocheo kikubwa kwake na kwa wanachama wengine wa CCM kujiamini kuwa ushindi uko karibu. 

Alisema serikali imeweka msingi mzuri wa maendeleo kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa katika sekta za afya, elimu, maji, miundombinu na uchumi wa viwanda.

"Rais wetu mpendwa Dkt Samia amefanya kazi kubwa na ya mfano tumeona utekelezaji wa miradi mikubwa ya barabara, hospitali, shule, na hata mikopo kwa vijana na wanawake Kama mwana-CCM, nimeona fahari kuwa sehemu ya mchakato huu wa kuleta maendeleo"

Huwel aliwaomba wananchi wote  kuendelea kuiamini CCM kwa kuwa ndiyo chama pekee chenye uwezo wa kuleta maendeleo ya kweli na ya kudumu. 

Alisema kwamba tofauti na vyama vingine ambavyo hujikita zaidi katika malalamiko, CCM imejipambanua kwa vitendo na utekelezaji wa ahadi zake.

“Wananchi wetu wanahitaji mbunge mwenye maono, anayejua vipaumbele vyao na anayejua namna ya kuvifikisha katika ngazi za maamuzi. 

Kuchukua fomu kwa Islam Huwel kunafanya idadi ya wana-CCM waliotangaza nia ya kuwania ubunge Iringa Mjini kuendelea kuongezeka, hali inayoashiria uchaguzi wa ndani wa chama hicho utakuwa na ushindani mkubwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI