Header Ads Widget

KAVEJURU ACHUKUA FOMU BUHIGWE, AOMBA KUTEULIWA TENA

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma.

Zoezi la uchukuaji fomu kwa wananchama wa CCM kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge katika majimbo mbalimbali mkoani Kigoma limeendelea kwa siku ya pili leo Juni 29  ambapo wanachama Zaidi walijitokeza kuchukua fomu.

Katika jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Felix Kavejuru amechukua fomu kuomba tena ridhaa ya kuteuliwa na CCM kugombea tena jimbo,

Kavejuru ambaye aligombea nafai hiyo kwenye uchaguzi mdogo mwaka 2021 baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Dk.Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Raisi wa Tanzania alieleza kuwa kuna kazi kubwa ambayo imefanywa na serikali hivyo anaomba ridhaa kuendelea pale alipoishia.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa CCM wilaya Buhigwe, Salum Hamisi Haji alisema kuwa kwa muda wa siku mbili ambazo wanachama wamechukua fomu hadi sasa jumla ya wanachama 13 wa CCM wamechukua fomu kuomba kupata ridhaa ya chama hicho kugombea ubunge katika jimbo la Buhigwe.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI