Header Ads Widget

MDAU WA MAENDELEO AIDAN MLAWA, ATIA NIA UBUNGE JIMBO LA KILOLO.

NA MATUKIO DAIMA APP.

KILOLO.Mfanyabiashara na Mdau wa Maendeleo jimbo la Kilolo Aidan Mlawa amechukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kilolo, Mkoani Iringa.

Akizungumza na wanahabari leo june 29,2025 baada ya kuchukua fomu Mlawa ameeeleza kuwa nia ya kugombea ni kutaka kuisaidia jamii pamoja na Dkt Samia  kwa kuwa jimbo la kilolo linahitaji kasi kubwa ya maendeleo.

"Kwa malengo na maono ya Rais wa Tanzania nimeona sina budi kujitoa na kwenda kushiriki naye ili pindi litakapotoka jina langu katika mapendekezo na kuteuliwa katika nafasi ya ubunge niweze kushiriki shughuli nzima za kimaendeleo na wananchi"

Alisema kuwa  ipo miradi mbalimbali ambayo inafanyika jimboni Kilolo inahitaji kusaidiwa na watu wenye weledi na wenye nia njema.

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI