Header Ads Widget

IRAN INA UWEZO WA KUANZA KURUTUBISHA MADINI YA URANIUM TENA - KWA UWEZEKANO WA KUNDA BOMU

 


Rafael Grossi anasema anatumai mazungumzo bado yanaweza kutokea katika siku zijazo, licha ya Iran kukata uhusiano na IAEA.

Iran ina uwezo wa kuanza kurutubisha madini ya uranium tena - kwa uwezekano wa kunda bomu- katika "muda wa miezi kadhaa", mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya nyuklia amesema. Rafael Grossi, mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya


Atomiki (IAEA), alisema mashambulizi ya Marekani katika maeneo matatu ya Iran mwishoni mwa juma lililopita yamesababisha uharibifu mkubwa lakini sio jumla, kinyume na madai ya Donald Trump kwamba vifaa vya nyuklia vya Iran "vimefutwa kabisa".


"Kusema ukweli, mtu hawezi kudai kwamba kila kitu kimetoweka na hakuna kitu hapo," Grossi alisema Jumamosi.


Israel ilishambulia maeneo ya nyuklia na kijeshi nchini Iran tarehe 13 Juni, ikidai kuwa Iran ilikuwa karibu kutengeneza silaha za nyuklia.


Baadaye Marekani ilijiunga na mashambulizi hayo, na kudondosha mabomu kwenye vituo vitatu vya nyuklia vya Iran: Fordo, Natanz na Isfahan.


Tangu wakati huo, kiwango cha kweli cha uharibifu hakijajulikana.


Siku ya Jumamosi, Grossi aliiambia CBS News, mshirika wa BBC wa vyombo vya habari vya Marekani, kwamba Tehran inaweza kuwa na "baada ya miezi kadhaa... misururu michache ya centrifuges inayozunguka na kuzalisha uranium iliyorutubishwa".


Aliongeza kuwa Iran bado ina "uwezo wa kiviwanda na kiteknolojia ... kwa hivyo ikiwa wanataka, wataweza kuanza kufanya hivi tena." I


AEA sio chombo cha kwanza kupendekeza kwamba uwezo wa nyuklia wa Iran bado unaweza kuendelea - mapema wiki hii, tathmini ya kijasusi ya Pentagon iligundua kuwa mashambulizi ya Marekani yalirudisha nyuma mpango huo kwa miezi kadhaa.


Trump alijibu kwa hasira kwa kutangaza kwamba maeneo ya nyuklia ya Iran "yameharibiwa kabisa" na kuvishutumu vyombo vya habari kwa "jaribio la kudhalilisha mojawapo ya mashambulizi ya kijeshi yenye mafanikio zaidi katika historia".


Kwa sasa, Iran na Israel zimekubaliana kusitisha mapigano. Lakini Trump amesema atafikiria "kabisa" kuishambulia Iran kwa mabomu tena ikiwa ujasusi utagundua kuwa inaweza kurutubisha uranium hadi viwango vinavyohusika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI