Header Ads Widget

TAKRIBAN WATU 81 WAMEUAWA KATIKA MASHAMBULIZI YA ISRAEL HUKO GAZA - HAMAS

 

Takriban Wapalestina 81 wameuawa na zaidi ya 400 kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel kote Gaza katika muda wa saa 24 hadi saa sita mchana Jumamosi, wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas imesema.

Katika tukio moja, takriban watu 11, wakiwemo watoto, waliuawa baada ya shambulizi karibu na uwanja wa michezo katika mji wa Gaza, wafanyakazi wa hospitali ya Al-Shifa na walioshuhudia waliambia mashirika ya habari.

Uwanja huo ulikuwa ukitumiwa kuwahifadhi watu waliokimbia makazi yao, wakiishi kwenye mahema.

Picha zilizothibitishwa na BBC zinaonyesha watu wakichimba mchanga kwa mikono mitupu na jembe kutafuta miili.

Jeshi la Israel lilisema "halikuwa na habari kuhusu majeraha kutokana na shambulio hilo" kando na "mtu anayeshukiwa alikuwa tishio" kwa vikosi vyake.

Wakati huo huo, Rais wa Marekani Donald Trump amesema ana matumaini usitishaji mapigano unaweza kuafikiwa wiki ijayo.

Wapatanishi wa Qatar walisema wanatumai shinikizo la Marekani linaweza kufikia makubaliano, kufuatia mapatano kati ya Israel na Iran yaliyomaliza mzozo wa siku 12 kati ya nchi hizo.

Mwezi Machi, usitishaji mapigano wa miezi miwili ulisambaratika wakati Israel ilipoanzisha mashambulizi mapya Gaza.

Mkataba wa kusitisha mapigano - ambao ulianza Januari 19 - ulilenga hatua tatu, lakini haukufanikiwa kupita hatua ya kwanza.

Hatua ya pili ni pamoja na kuanzishwa kwa usitishaji vita wa kudumu, kurejea kwa mateka waliosalia huko Gaza badala ya Wapalestina waliofungwa nchini Israel, na kuondolewa kabisa kwa majeshi ya Israel kutoka Gaza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI