Baadhi ya Walimu wa ajira mpya wa Elimu ya biashara na Amali wakisikiliza wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu kwa Walimu hao wapya wa masomo ya Elimu ya biashara na Amali kwa shule za sekondariza Serikali Tanzania bara
Naibu katibu mkuu Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Daniel Mushi akifungua mafunzo ya Walimu ajira mpya ya Elimu ya biashara na Amali mkoani Morogoro.Lilian Kasenene
Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio Daima Media
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iimeandaa mpango madhubuti wa kuwasomesha bure walimu 1,699 wa ajira mpya ili waweza kujiendeleza kupitia Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania,
Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Daniel Mushi alieleza hayo mbele ya Walimu wa ajira mpya katika mafunzo maalumu kwa Walimu hao wapya wa masomo ya Elimu ya biashara na Amali kwa shule za sekondariza Serikali Tanzania bara
Prof. Mushi alisema Serikali pamoja na mambo mengine Mpango huu utahusisha kuwalipia ada katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na mpango uliopo ni kuwa katika kipindi cha miaka mitano kila mwalimu ajiendeleze akiwa katika kituo chake cha kazi.
"Ili muweze kuhitumu mafunzo ya Post-Graduate Diploma in Education mkiwa kazini Tena vituo kwenu mtapata hiyo ellimu bure na mmepewa muda mrefu wa kujifunza,"alisema.
Alisema Lengo ni kuhakikisha kuwa walimi hai wanapata vigezo stahiki vya utumishi wa umma kama walimu ndani ya miaka mitano,na kwamba Serikali inatambua walimu kama taaluma nyingine wanahitaji kupata mafunzo ya mara kwa mara ndio maana imeweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA)ni lazima na siyo hiari kwa walimu wote nchini wa shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Aidha aliwatakq kutumia fursa hiyo kupata ujuzi na maarifa katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Elimu ya Biashara na Amali pamoja na kubadilishana uzoefu kujiwekea mikakati ya namna ya kutumia ujuzi watakao upata ili kuleta mabadiliko chanya katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji na kuimarisha umahiri utakaojengwa kwa wanafunzi.
Katika kuimarisha sekta ya elimu kwa kuwekeza kwenye rasilimali watu hususan walimu Serikali iliridhia ajira ya walimu wapya 4,633 kati yao 4,075 wa masomo ya Biashara na 558 ni wa masomo ya Amali,hatua hiyo muhimu ya kisera ni kielelezo cha jinsi ambavyo Serikali inajali ubora wa elimu na ustawi wa vijana.
"Kuanzishwa kwa masomo ya Elimu ya Biashara na Amali kumepelekea uhitaji mkubwa wa walimu na ndiyo maana Serikali ilitoa kibali cha kuajiri walimu hao na kutoa rasilimali fedha za kuwezesha mafunzo ya walimu hawa,"alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET)Dk Aneth Komba,alisema jumla ya sh Bilion 2.5 zimepangwa kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo na fedha hizo ni za kufanikisha utoaji wa mafunzo kwa walimu wa ajira mpya wa masomo ya Amali na Elimu ya Biashara kwa Mwaka wa Fedha pamoja na fedha nyingine ambapo TET imepokea.
Dk Komba alisema jumla ya walimu wa ajira mpya 660 kati ya 1699 kutoka katika shule za Sekondari zilizopo katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Lindi, Mbeya, Mtwara, Songwe, Njombe, Ruvuma, Manyara na Singida wanaendelea na mafunzo ya siku 10 katika Chuo cha Ualimu Morogoro.
Aidha, mafunzo yanatolewa katika vyuo vitatu ambavyo ni Chuo cha Ualimu Tabora wepo washiriki 630, Chuo cha Ualimu Morogoro walimu 660 na Chuo cha Ualimu Korogwe kitakuwa na washiriki 409.
Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 pamoja na Mitaala iliyoboreshwa ya mwaka 2023.
MWISHO..
0 Comments