Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MBUNGE wa Jimbo wa la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew amewapongeza Madiwani wa Kata za Sima, Malambo, Bariadi na Somanda kwa kusimamia miradi ya Maendeleo pamoja na shughuli za Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mhandisi Kundo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, ameyasema hayo kwenye Mkutano Maalumu wa kuwasilisha Utekelezaji wa Ilani ya CCM (2020/2025) uliofanyika Shule ya Sekondari Kusekwa Memorial Mjini Bariadi, Mkutano ambao umehusisha viongozi wa CCM kutoka Kata za Malambo, Sima, Bariadi na Somanda.
Amewapongeza Madiwani hao kwa kusema kuwa wamekuwa kiungo muhimu kwa kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kusimamia Utekezaji wa Ilai katika sekta za Elimu, Afya, Maji, Umeme, Barabara na Miundombinu mingine.
"Madiwani mmekisaidia sana Chama Cha Mapinduzi katika Utekelezaji wa Ilani ya CCM...Mmekitendea haki chama kwa falsafa ya mafiga matatu ya CCM, Maendeleo yanatokana na fedha za Serikali Kuu ya Halmashauri, nawashukuru sana Madiwania kwa kusimama kidete kusimamia fedha za miradi ya Maendeleo" amesema.
Mhandisi Kundo amewaambia Wana CCM kuwa waliwaletwa Madiwani ambao wanasimamia miradi ya Maendeleo ambapo kila kata kuna miradi ya Maendeleo imetekelezwa na nyingine zinaendelea kutelekezwa.
"Mlituletea watu wanaosimamia miradi ya Maendeleo ambapo kila kata Kuna miradi imetekelezwa...Nawashukuru sana kwa imani mliyoweka kwangu na Madiwani, wakati nakabidhiwa kitabu (Ilani) yenye kurasa zaidi ya 300, tumetekekeleza vilivyo na nafahamu Bariadi tuliyokuwa nayo na ninahafahamu Bajeti ya kila kata" amesema na kuongeza.
" Mapinduzi yaliyofanyika ni lazima tumshukuru Rais Dkt. Samia, Wana Bariadi tutaendelea kumshukuru Rais Dkt. Samia na hayo yaliyofanyika ni sauti ya Wana Bariadi waliyohitaji tuyafanye."
0 Comments