NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Taasisi ya CHAMATA ASSOCIATION yakabidhi mitungi ya gasi 300 kwa makundi maalumu mkoani Morogoro ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhimarisha matumizi ya nishati safi nchini ili kutunza mazingira.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya CHAMATA ASSOCIATION Peter Ngwele,akizindua kampeni hiyo kitaifa mjini Morogoro amesema lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu ya umuhimu wa kutumia nishati safi dhidi ya nishati chafu nchini, kampeni hii wameipa jina NISHATI SAFI NA SAMIA, na kauli mbiu ikiwa "JIKO SAFI - MAPISHI SAFI".
"Tumekabidhi 300, malengo kukabidhi 100,000 kwa nchi nzima Kwa mama lishe, Walemavu, wazee, vikundi vya vijana wenye mradi wa chakula."
Lengo la kampeni hii ni muendelezo wa kazi nyingi ambazo Taasisi ya CHAMATA ASSOCIATION imekuwa ikizifanya katika kuunga mkono Juhudi kubwa zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan, ikiwemo kuelezea miradi,kutoa elimu ya urai, amani na maswala ya Uchumi.
Katibu Mkuu huyu aliambatana na mweka hazina Taifa ndugu Edmond Ernest walipofika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mjini Musa Kilakala kwa ajili ya kujitambulisha na kuzungumza na waandishi wa Habari.
Katibu Mkuu wa CHAMATA ASSOCIATION, alielezea ya kuwa wanafurahi sana na kujivunia kwa kuwa kinara wa kampeni hii Africa na Duniani kote ni Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan, hivyo tunakila sababu ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya mfano Duniani Kote kwa matumizi ya nishati safi.
Kampeni hii itakwenda kuhakikisha wananchi wengi wanahamia kutoka kwenye nishati chafu (Kuni na mkaa) kwenda kwenye nishati safi, hii itakuwa na faida nyingi sana kwa Taifa letu. Mosi, tutaokoa misitu yetu kupotea kwa ukataji holela wa miti kwa ajili ya Kuni na mikaa,
"Pili tutavilinda vyanzo vya maji kupotea, tatu,kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Nishati safi pia itawasaidia watumia kutumia muda mchache kwenye maandalizi ya chakula, kuepukana na maradhi yatokanayo na moshi utakao kwenye nishati chafu" alisema.
Peter amesema kampeni hii imekusudia kufikia mikoa mitano kwa kuanzia ambayo ni Morogoro, Geita, Dodoma, Manyara na Kigoma kwa kuanzia lengo ikiwa kufikia nchi nzima.
Aidha amesisitiza watanzania wote kushiriki uchaguzi ujao kwa amani na kuhakikisha wanamchagua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ilikuendeleza kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi Cha miaka minne ya Uongozi wake.
0 Comments