Header Ads Widget

MBUNGE KAVEJURU AWATAKA WAPIGA KURA WATOE HUKUMU YA HAKI

 

Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Shaban Ng'enda

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MBUNGE wa jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma Felix Kavejuru amewataka wapiga kura katika jimbo hilo  kutoa maamuzi ya haki katika kuwachagua wana CCM wanaowania kugombea ubunge kwenye uchaguzi Mkuu mwaka huu.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Bukuba wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Mbunge huyo alisema kuwa wapiga watoe maamuzi yanayozingatia uhalisia wa mtu ambaye kwa hakika anawiwa kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo.



Kavejuru ambaye ametangaza kugombea tena ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu mwaka huu alisema kuwa kama wapiga kuwa watatenda haki anayo nafasi na vigezo vya kurudi tena kuwahudumia wananchi wa jimbo hilo kwa kazi kubwa aliyofanya ambapo amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka minne.


Hadi sasa wanachama wa CCM 14 wameonesha nia ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kwenye jimbo hilo kupitia CCM wakisubiri kuanza mchakato wa uchuakuaji fomu Juni 28 mwaka huu.


Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda  akizindua Zahanati ya Bangwe Manispaa ya Kigoma Ujiji ameeleza azma yake ya kugombea tena ubunge katika jimbo hilo ambapo alisema kuwa kazi kubwa imefanyika kwa kipindi cha miaka mitano aliyokuwa mbunge katika jimbo hilo.



Ng’enda ameomba tena ridhaa ya wananchi wa jimbo hilo  kugombea tena akikabiliwa na mchuano  kutoka kwa wanachama wa CCM akiwemo Msanii na Mtangazaji wa Wasafi FM,Clayton Revocatus maarufu Baba Revo, Baruani Muhuza kutoka Azam Media.


 Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI