Na Lilian Lucas,Morogoro
Habari na Matukio App
THE Healing Missionaries(THM) ya jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na kundi la muziki wa injili la Armee seben la mkoani Morogoro itafanya mkutano wa injili wenye nia ya kuombea Amani nchi ya Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu pamoja na maombi maalumu kwa vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro mchungaji msaidizi wa huduma ya The Healing Missionaries(THM) Pasta Patrick Mulunda alisema mkutano huo ni wa injili ambao utaambatana na maombi na maombezi na ni kitu cha kipekee katika kuhamasisha vijana kumjua mungu.
Alisema mkutano huo wa injili utajulikana kama Seven In Christ Season na ni ibada itakayo waunganisha watanzania hususani vijana ambao wamekuwa wakijisahau ama kutofikiwa kwa ukaribu hasa kwenye eneo la kumwabudu Mungu.
“MUNGU aliibariki hiyo siku ya saba na kuitakasa hii namba ni ya ukamilifu, hii namba saba imetumika kwenye vitabu vingi vya Biblia ikiwemo kitabu cha Ufunuo imetumika zaidi ya mara hamsini na katika muktaza wake tunaona barua saba kwa ajili ya makanisa saba huko Asia na roho sana katika kiti chake cha enzi imekutika kama malaika saba,”alisema.
Alisema waliona kutumia siku hiyo ya Julai saba kwa sababu ni namba ya ukamilifu,ambapo aliwaomba wananchi wa Morogoro kujitokeza kushiriki katika mkutano huo kwa ajili ya kumsifu,kumwabudu,kupiga kelele kuu kwa Mungu ili kuhakikisha suala la uchumi, afya na elimu kujidhihilisha.
Kwa upande wake katibu wa THM Sarah Mpangala alisema wameamua kuandaa ibada hiyo(mkutano) kufanyia katikati mji ili kuwafikia wananchi wote ambao mara nyingi uwa makazini na hawapati nafasi ya kushiriki ibada siku ya jumapili na hiyo itakuwa nafasi kwao.
“Eneo tutakalofanyia ibada kwa sababu wengi wako makazini,kwa hiyo tumesema twende ili kuwapata wafanyakazi na wafanyabishara pamoja na kuwavuta vijana ili kumwabudu na kumsifu Mungu kwa pamoja,”alisema Mpangala.
Mkurugenzi wa Armee Seben Meshack Shetente alisema kwa mazingira yoyote watahakikisha wanawafikia watu kwani kuna baadhi hawasikii neon la mungu na kusudio ni kuhubiri kwenye mazingira yote.
Kabla ya kufanyika kwa mkutano huo wa injili THM na Armee Seben watatembelea vituo vya mahitaji maalumu wakiwemo watoto yatima kwa kula na kucheza nao.
Ibada ya mkutano huo itahudhuliwa na Bishop Emmanual Mgaya maarufu Masanja Mkandamizaji pamoja,Hellen Majeshi maarufu Rubby, Kibonge wa Yesu na kwaya na waimbaji mbalimbali kutoka jijini Dar Es Salaam na Morogoro.
Mwisho.
0 Comments